JIHADHARI NA UTAPELI HUU KWENYE MIRADI YA UJENZI INAYOENDELEA.

Siku hizi, tofauti na miaka ya nyuma kidogo miradi ya ujenzi imekuwa ikihiatajika kupata usajili katika taasisi na bodi mbalimbali zinazojihusisha na ujenzi pamoja na mawakala wao. Mabadiliko ya sheria na taratibu yamekuwa yakitokea mara kwa mara na taasisi hizi zimezidi kufanya ufatiliaji mkali zaidi siku hadi siku kuhakikisha kila mradi wa ujenzi unafuata taratibu zote za kisheria kwa kutumia mawakala wao, pamoja na watu wao wenyewe kutokea ofisini kwao.

Lakini hata hivyo, pamoja na yote hayo bado miradi mingi ya ujenzi imekuwa haisajiliwi kwa sababu mbalimbali, nyingine za msingi na nyingine zisizokuwa za msingi. Mradi wa ujenzi unaweza kuwa tayari umeanza lakini bado haujasajiliwa kwa sababu labda vibali na vielelezo muhimu vilichelewa kuwasilishwa, au kumekuwa na ukwamishaji kwa sababu kuna utaratibu haujakamilika, au inawezekana mradi husika haujafikia viwango vya kusajiliwa katika taasisi husika, au wakati mwingine mteja mwenyewe hataki kuusajili kwa sababu anakwepa gharama kubwa za usajili huo au sababu nyingine yoyote ambapo watu wa mamlaka husika wakipita katika eneo la ujenzi na kukuta mradi huo haujasajiliwa watachukua hatua dhidi ya mradi husika.

KUNA SABABU NYINGI ZA MRADI KUTOSAJILIWA AU KUCHELEWA

Kwa sababu hizo limetokea kundi kubwa la matapeli ambao wanapita kwenye eno lolote ambapo ujenzi unaendelea wakiw ana barua na baadhi ya vielelezo vingine feki wakijitambulisha kwamba ni watu kutoka mamlaka husika wanaofuatilia kuangalia kama mradi umepitia hatua zote muhimu na kwamba wameona mradi huo umekiuka taratibu hivyo wametaka kukupeleka kwenye mamlaka husika ukapewe adhabu ya kupigwa penati pamoja na kufuata taratibu. Baada ya kukukabidhi barua na kukutajia fedha nyingi sana ambazo utahitajika kulipa kama adhabu ya kukiuka taratibu husika wanachukua mawasiliano yako kisha baadaye wanakupigia simu na kukwambia uwape rushwa kiasi fulani ili wakafute kesi hiyo na kukulinda mpaka mradi umalizike. Sasa kujua kama watu hao ni matapeli au sio matapeli unapaswa kuwa na mtu mzoefu anayeelewa taratibu husika na anayeweza kufanya ufuatiliaji kuhakikisha kama watu hao ni kweli wametumwa na mamlaka husika.

ANAHITAJI MTAALAMU SAHIHI MWENYE UZOEFU KUJUA MATAPELI NA WASIO MATAPELI

Watu wengi sana wametapeliwa na wanaendelea kutapeliwa na watu ambao hawatoki kwenye mamlaka husika na kujikuta wakilipa fedha nyingi au rushwa kubwa kwa watu ambao sio sahihi, tumeshakutana na baadhi ya kesi hizi na wengi wametapeliwa kwa sababu hawana uzoefu wala utaalamu wa kutosha kwenye fani ya ujenzi kugundua tofauti kati ya watu sahihi na matapeli.

WATU WENGI WAMETAPELIWA NA WANAENDELEA KUTAPELIWA KWA KUSHINDWA KUWAELEWA MATAPELI HAWA

N:B Wapo watu kutoka kwenye mamlaka husika ambao hufuatilia miradi inayojengwa kuhakikisha kwamba imefuata taratibu husika, lakini changamoto ni kwamba wimbi la watu matapeli limeongezeka sana miaka ya karibuni hivyo ni muhimu kufahamu hili na kuwa na mtu wa karibu anayeweza kukusaidia kuhakikisha kama watu hao ni matapeli au ni kweli wanawakilisha mamlaka husika wanayosema wametokea.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *