UWIANO KWENYE UJENZI KATI YA GHARAMA YA KUJENGA NA GHARAMA YA KUMALIZIA(FINISHING)

Kati ya vitu vyenye utata mkubwa na ambavyo haijawahi kueleweka na kuzoeleka ni gharama sahihi za ujenzi. Utata huu unachangiwa na mambo mengi na kwa watu wengi ni ngumu kuona kwa sababu inahitaji mtu awe anafikiri sana kuweza kuona utata ulipo. Gharama za ujenzi haziwezi kueleweka moja kwa moja kwa kuna tofauti nyingi sana ndogo ndogo kati ya mradi mmoja na mwingine kama vile utofauti ukubwa wa mradi ambapo sio rahisi mradi mmoja na mwingine ilingane kwa kila kitu na utofauti huo ndio unaoleta tofauti ya bei, pia kuna utofauti wa gharama za malighafi ambazo mteja amechagua kununua ambapo kuna utofauti mkubwa wa bei kadiri ya ubora wa vifaa husika vya ujenzi. Mambo mengine ni kwamba kuna asili ya kijiografia ya eneo husika, kuna viwango tofauti vya gharama za ufundi wa mradi husika, kuna wingi wa urembo na vipengele vya madoido katika jengo n.k.,

NUSU YA KWANZA YA UJENZI INAFIKA MPAKA KUPAUA

Lakini sasa, licha ya sababu zote tulizoorodhesha hapo juu gharama za ujenzi unaweza kuamua kuzitafutia uwiano katika sehemu mbili kuu. Sehemu ya kwanza ni gharama za kujenga jengo mpaka kupaua kabla ya kuingia hatua ya umaliziaji(finishing) na sehemu ya pili ni gharama za umaliziaji kutokea hatua ya jengo kupauliwa mpaka kumalizika na kuanza kutumika ambapo gharama ya umaliziaji(finishing) imebeba hatua zote za huduma katika jengo kama vile umeme, viyoyozi, mfumo wa maji taka na vingine vinavyoendana na hivyo, vipendele vya urembo na muonekano pamoja na umaliziaji wa kuta na sakafu na mengineyo.

NUSU YA PILI INAKAMILISHA UMALIZIAJI WA KILA KITU KABLA YA JENGO KUHAMIWA

Sasa ni kwamba sehemu hizi mbili za hatua za ujenzi uwiano wa gharama zake ni wastani wa nusu kwa nusu. Yaani gharama ya mradi mzima kwa wastani huwa nusu ya gharama huenda kwenye hatua ya ujenzi mpaka kufikia kupaua na nusu nyingine ya gharama huenda kwenye hatua ya umalizia(finishing), huo ndio wastani wa uwiano wa gharama za ujenzi kwa hatua hizo mbili kubwa.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *