USIPUUZE UTAALAMU MAKOSA KWENYE MRADI WA UJENZI NI UHAKIKA – 1.

Watu wengi wamekuwa wakijdanganya kwamba wanaweza kuweka umakini wa kutosha kuepuka makosa yoyote ya kiufundi yanayoweza kujitokeza na kuharibu mradi ujenzi. Lakini ukweli ni kwamba hata miradi mikubwa kabisa yenye idadi kubwa kabisa ya wasimamizi na inayofuata itifaki iliyopangiliwa kwa usahihi bado hujikuta ikiwa na makosa kiasi. Hivyo ni kujidanganya kwamba unaweza kuyaondoa peke yako kwa kuweka umakini.

Japo la kwanza na muhimu la kuhakikisha makosa yanapungua kwa kiasi kikubwa ni kuweka usimamizi na ukaguzi wa mradi mara kwa mara wa mradi huo. Kwa uzoefu wangu binafsi hakuna mradi wowote ujenzi ambao hauna usimamizi wa kitaalamu ambao haujakutana na makosa makubwa kabisa muhimu kabisa. Hii ni kwa sababu kuna makosa makubwa ya kitaalamu ambayo yanaweza kuonekana kwa haraka na mtaalamu peke yake na watu wengine wasione kiurahisi au wakapuuzia wakati ni kosa kubwa.

Kwa mfano kuna mradi mmoja wa jengo la ghorofa ambao michoro ya ramani ilianza kufanyika kisha mradi ukaenda kufanyika kwa hatua ya kuseti jengo na kuanza kuchimba na kujenga msingi. Mtaalamu amefika eneo la ujenzi wakati ambao kuta za msingi zimeshapandishwa na ndipo wanakaribia kuanza kazi ya kurudishia udongo. Lakini akakuta tayari makosa makubwa yamefanyika ambapo uelekeo wa jengo husika umefanyika kimakosa, kwani jengo lilipaswa kutazama upande tofauti ili lilipowekwa kutazama ili lilete ule mwonekano bora uliokusudiwa hususan upande wa mbele.

Lakini kwa sababu jengo lilishafika hatua ya mbele sana na msingi unakaribia kuisha na hivyo kuvunja na kuanza upya ili jengo lielekezwa mwelekeo sahihi ni kitu kisichowezekana kiurahisi tena. Kosa kubwa lililofanyika hapo ni kukosekana kwa msimamizi wakati wa setting ambaye angeliona tatizo kwa haraka sana kama jinsi alivyoliona mara tu alipofika site na hivyo angetaka yafanyike marekebisho kitu ambacho wengine waliokuwa wanafanya kazi yote jiyo hawakuweza kuona kabisa.

Changamoto za namna hii zinazosababishwa na kukosekana na mtaalamu sahihi katika eneo la ujenzi ni nyingi zinakuja na gharama kubwa sana kwa mradi husika wa ujenzi. Hivyo ni muhimu mno awepo mtu makini wa kuhakikisha akitazama kwa mwonekano wa jicho la kitaalamu aone kila kitu kinaenda sawa kabisa.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *