HUDUMA ZETU

Tunatoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwenye ujenzi kuanzia upatikanaji wa ramani, vibali vya ujenzi, usimamizi wa ujenzi na hata mafundi bora wa kuaminika na wa uhakika

TUNAANDAA MICHORO

Tunandaa aina zote za michoro kama ifuatavyo

-Architectural drawings
-Structural Engineering drawings
-Interior designs

Pia tunafanya makadirio ya gharama za ujenzi.

TUNATOA USHAURI

Tunatoa ushauri wa hatua sahihi za kufuata kabla ya ujenzi kuanza na hata kabla ya michoro kuanza ili kuwa na ujenzi wenye mafanikio na kuepuka changamoto na majuto baada ya mambo kuharibika

Tunatoa ushauri pia kwa mradi ulioharibiwa kabla ya kumalizika au uliomalizika lakini umeanza kuleta matatizo.

TUNASIMAMIA

Tunasimamia ujenzi kama washauri wa kitaalamu (post-contract consultants)

Tunasaidia kuzungumza na mamlaka husika kutatua changamoto na kutokuelewana kati ya mamlaka husika na mteja.

Tunakikisha mradi unajengwa kwa ubora wa hali ya juu.

TUNATEMBELEA SITE

Tunatembelea site ya ujenzi ili kutoa suluhisho changamoto yoyote ambayo inaukabili mradi husika.

TUNASHUGHULIKIA VIBALI

Tunashughulikia vibali vyote vya ujenzi kutoka mamlaka husika kuanzia halmashauri, stika za bodi za ujenzi, zimamoto, osha, n.k., kwa kuzingatia masharti yao

TUNAJENGA

Tunatoa huduma ya ujenzi bora kabisa kwa miradi ya aina zote unaziongatia viwango bora, uimara wa jengo, na umaridadi wake.