Paa za makuti ni moja kati ya ubunifu wa mwanzo kabisa wa uezekaji wa binadamu na bado linaendelea kutumika sana duniani kote mpaka leo hii. Makuti haya ambayo mara nyingi huwa yametengenezwa na majani makavu huenda juu kwa pembe ya nyuzi 45 na kutengeneza mteremko mkali na kuwa na unene wa kufikia mita 0.4 au hata zaidi. Unene huu hujumuisha matabaki kadhaa ya majani mazito. Matabaka haya huhakikisha maji ya mvua hayapenyi ndani ya nyumba na ukali wa mteremko wa paa husaidia maji kuondoka kwenye pa ana kumwagika chini haraka kabla hayajapenya ndani ya nyumba.

FAIDA ZA PAA ZA MAKUTI

-Paa za makuti zinadumu miaka mingi, zinakadiriwa kufikisha hata miaka 70 kabla ya kuzeeka na kubadilishwa ikiwa umetumia malighafi sahihi.

-Paa za makuti zinapunguza ukali wa hali ya hewa ya ndani ya nyumba ukilinganisha na hali iliyoko nje, wakati wa joto kali paa za makuti zinatunza ubaridi ndani ya nyumba na wakati wa baridi kali paa hizi zinatunza joto ndani ya nyumba.

-Paa za makuti zinafaa kutumika kwa kuchanganywa na aina nyingine za paa ili kuongeza manufaa yanayopatikana kwa kutumia paa la makuti pamoja nap aa nyingine

-Paa za makuti ni nyepesi na hivyo zinapunguza mzigo unaobebwa na jengo na matokeo yake kupunguza gharama zenyewe za jengo.

CHANGAMOTO ZA PAA ZA MAKUTI

-Kunahitajika nguvu kazi kubwa sana na muda mwingi kuezeka paa za makuti kwani ni kazi kubwa sana kuezeka paa la makuti mpaka kukamilisha na inahusisha watu wengi hivyo gharama ya nguvu kazi pia ni kubwa.

-Paa za makuti zinahitaji ukaguzi wa mara kwa mara au kukaguliwa na mtalaamu angalau mara moja kwa mwaka kuhakikisha hakuna uharibifu wowote unaoweza kuleta usumbufu kwa watumiaji wa jengo husika.

-Paa za makuti zinahitaji ukarabati wa mara kwa mara au matengenezo kwani tatizo la paa kuvuja ni tatizo ambalo hujitokeza zaidi katika mapaa ya makuti.

-Paa za makuti zinahitaji umakini kwenye kuzilinda na hatari mbalimbali kama vile moto, kushambuliwa na wadudu, unyevu na kuzilinda dhidi ya radi.

NOTE: Muhimu kukumbuka kwamba ubora wa paa za makuti unatokana na ubora wa muezekaji, ni muhimu sana pia kupata ushauri kutoka kwa mwezekaji bora kabisa juu ya uezekaji wa paa la makuti na malighafi sahihi kabla ya kuanza kufikiria kuezeka.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790