PAA LA MABATI
-Uezekaji wa mabati ndio uwezekaji ambao ni maarufu zaidi katika zama hizi tunazoishi sasa. Uezekaji wa mabati unatumika katika kila aina ya majengo na miradi ya ujenzi mikubwa kwa midogo. Paa la mabati ni jepesi, imara, linapatikana kwa bei nafuu, halipitishi maji kabisa na linapatikana katika aina nyingi sana.
FAIDA ZA PAA LA MABATI
-Paa la mabati ni jepesi sana, paa la mabati ni jepesi ukilinganisha na aina zote za mapaa ya vigae hivyo linasaidia sana katika kupunguza uzito wa mzigo wa paa na kuepusha gharama za kuimarisha jengo ili liweze kumudu mzigo wa paa kama vile kuongeza au kuimarisha nguzo.
-Paa la mabati ni rahisi kuezeka na linatumia muda mchache ukilinganisha na mapaa mengine kama vile vigae kwa sababu kipande kimoja kinachukua eneo kubwa la mraba na ni jepesi sana kunyanyua na kuezeka.
-Paa la mabati linaakisi mwanga hivyo ni rahisi kuzuia kuondoa mwanga wa jua kuja moja kwa moja ndani ya jengo na hivyo kupunguza joto ndani ya nyumba.
-Paa la mabati linadumu kwa miaka mingi kufikia takriban miaka 50 bila kubadilishwa licha ya kuwa jepesi sana ukilinganisha na mapaa ya vigae.
-Paa la mabati linahimili hali za hewa zinazoweza kuleta uharibifu kama vile mvua kubwa, upepo mkali, barafu inayoanguka n.k.,
-Paa la mabati pia linazuia uharibifu kama vile ajali ya moto, kushambuliwa na wadudu waharibifu kama vile mchwa na kuepuka kuoza.
CHANGAMOTO ZA PAA LA MABATI
-Paa la mabati ni gharama kubwa, japo linadumu kwa muda mrefu huku likihusisha ukarabati mara chache hivyo kuwa na nafuu kwa baadaye lakini gharama za mwanzoni za paa la mabati ni kubwa sana.
-Paa la mabati wakati mwingine husababisha kelele wakati wa mvua kitu ambacho huleta usumbufu kwa baadhi ya watu japo watu wengine hufurahia kelele za aina hiyo.
-Paa la mabati huwa vigumu kutembea juu yake hasa wakati wa mvua au unyevu kwani huteleza sana lakini pia mabati ni laini kiasi cha kukunjika kama utakanyaga vibaya.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!