Entries by Ujenzi Makini

KUENDELEZA NYUMBA ILIYOPO NA KUCHORA RAMANI UPYA.

Katika kufanya kazi za ramani za nyumba kuna watu wengi ambao wanahitaji ramani mpya kabisa kwenye kiwanja kipya lakini kuna watu wachache ambao wao wanahitaji kuendeleza nyumba ambayo tayari ipo katika eneo husika aidha kuifanya kuwa kubwa zaidi au kuifanya kuwa ya ghorofa kabisa. Hata hivyo kazi hizi zote zinafanyika kwa namna tofauti na ile […]

KWENYE UJENZI UADILIFU BINAFSI NA MAADILI YA KAZI YA MJENZI/MKANDARASI MWENYEWE NDIO MUHIMU ZAIDI.

Changamoto zinazotokana na miradi ya ujenzi ni nyingi sana hususan miradi ambayo inafanyika bila kufuata taratibu zote za kitaalamu ambazo zimewekwa kwa lengo la kuhakikisha kwamba mradi unafanyika kwa mafanikio na kupunguza sana hatari ya kupata hasara, mradi kushindwa kumalizika kwa wakati, kazi kuwa ya viwango duni au uzembe unaoweza kupelekea uharibifu na usumbufu. Uhalisia […]

WAMILIKI WA MAJENGO KARIAKOO MSISUBIRI SERIKALI KAGUENI MAJENGO YENU WENYEWE.

Wakati tunaendelea na maombolezo ya maafa ya kuanguka kwa jengo la ghorofa nne katika mtaa wa mchikichini Kariakoo na kupelekea vifo vya watu ambao idadi yao inasemekana kufikia 13 mpaka sasa huku majeruhi wengi wakiendelea kutibiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili serikali imeshaunda kamati ya kufanya uchunguzi wa majengo yote ya Kariakoo. Katika hali […]

WAMILIKI WA MAJENGO KARIAKOO MNAMSIKILIZA NANI?

Imekuwa ni hali ya kawaida pale mtu anapotaka kujenga kwanza huwa anaanza na kujaribu kushirikisha wale watu wa karibu wanaomzunguka kupata mawazo na maoni yao juu ya kile anachokwenda kufanya. Mara nyingi huwa ni marafiki wa karibu na hasa wale ambao tayari wana uzoefu binafsi katika miradi ya ujenzi kama huo anaoenda kufanya. Lakini pia […]

WAMILIKI WA MAJENGO KARIAKOO WACHUNGUZE MAJENGO YAO.

Wataalamu wengi wa hapa Tanzania hasa wale wataalamu makini na wanaojali kuhusu sifa zao na sifa za makampuni yao kwa maana ya wasanifu majengo, wahandisi mihimili wa majengo, wakadiriaji majenzi wa majengo pamoja na baadhi ya wataalamu wengine, wanapoitiwa mradi unaoenda kujengwa Kariakoo huwa wanaikataa au kuiagizia kwa watu wengine wasiojua au kujali sana kuhusu […]

HII NDIO SABABU KUU YA GHOROFA KUANGUKA KARIAKOO.

Kabla sijaingia ndani kuanza kuchambua sababu ambazo hupelekea maghorofa kuanguka niende moja kwa moja kueleza sababu kuu ili hata wale ambao hawatasoma zaidi basi wawe wametoka na kitu kimoja kikubwa. Sababu kuu ya ghorofa kuanguka ni kukosekana kwa usimamizi makini wa wataalamu au maelekezo yao kupuuzwa bila ya wao wenyewe kujua kama yalipuuzwa endapo hakusubiri […]