CHANGAMOTO YA NYUMBA ZA “CONTEMPORARY” MAARUFU KAMA PAA LISILOONEKANA
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la watu kupenda aina mbalimbali za “design” za nyumba huku staili ya aina ya contemporary ikipata umaarufu mkubwa kwa baadhi ya watu. Staili hii imekuwa ikipendwa sana kwa sababu ya kuvutia kwake kutokana na ule mpangilio wa “perspective lines” zinazokwenda sambamba kutokea chini mpaka kwenye paa huku paa lenyewe ambalo lina pembe ndogo sana likiwa halionekani kwa sababu linakuwa limefichwa na kuta za “parapet walls”. Baadhi ya watu wamekuwa wakiiona staili hii kuwa ndio ya kisasa zaidi na inayokwenda na wakati.
Lakini kama tunavyoijua sheria ya asili kila kizuri hakikosi changamoto yake, hivyo kutokana na kwamba paa la kwenye hizi “contemporary style houses” huwa linatumbukia ndani na linafichwa na kuta za “parapet walls” maji ya mvua yanayoangukia kwenye paa hutitirika na kumiminikia kwenye “gutter” ya zege maarufu kama “concrete gutter” ambayo ndio huyakusanya na kuyapeleka kwenye bomba linaloyashusha chini ardhini maarufu kama “vertical storm water duct” na kupelekwa sehemu iliyokusudiwa. Changamoto ambayo hutokea mara nyingi ni kwamba, zege hili la “concrete gutter” mara nyingi halisafirisha maji yote kuelekea kwenye “vertical duct” badala yake baadhi huanza kidogo kidogo kupenyeza ndani ya zege na baada ya muda huanza kuonekana kwa ndani ya nyumba kuwa yanavuja.
Watu wengi wasichojua ni kwamba maji huwa yana nguvu sana na yana ubishi wa hali ya juu pale yanapopata eneo lenye udhaifu au upenyo wa aina yoyote ile wa kupenyeza, hukazana sana hata kama sio kwa haraka lakini baada ya muda huanza kuonekana madhara yake. Sababu kuu ya kwa nini maji haya hufanikiwa kupenyeza ni kwa sababu wanaojenga hawajua vizuri nguvu ya maji haya baada ya muda mrefu hivyo hawaweki uzito wa kutosha na ubunifu wa hali ya juu kwenye sehemu hii na kwa sababu itachukua muda kidogo kuja kuonekana, makosa haya hayaonekani mapema na hivyo inakuja kuwa ni changamoto kubwa baadaye.
Kutokana na changamoto hii baadhi ya watu wameanza kuogopa haya mapaa ya nyumba hizi za staili ya “contemporary” na kuamua kurudi kwenye mapaa marefu yaliyozoeleka. Hata hivyo suluhisho la changamoto hii ni ufundi sahihi ambao bado ni mafundi wachache sana ambao wanafanya kazi kisasa na kisayansi ndio wanaweza kukabiliana nayo. Usahihi wa ufundi kwa changamoto hii ni pamoja na kuzingatia sana zege ya “concrete gutter” ambayo ni waterproof, yenye mteremko sahihi na yenye “finishing” laini kama ya vigae vya sakafuni(floor tiles).
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Napenda sana nyumba ya Contemporary nahitaji ufahamu zaidi kuziusu kabla sijaanza ujenzi.
Karibu sana
Whatsapp/Call +255717452790.