UJENZI WA HARAKA(FAST TRACK CONSTRUCTION)
Ujenzi wa haraka au “fast track construction” namna ya ufanyaji ujenzi ambapo ujenzi unaanza hata kabla ya michoro kukamilika. Lengo la ujenzi kwenda haraka ni ili kupunguza muda wa kukamilisha ujenzi husika.
Njia hii ya kufanya ujenzi kwa haraka huwa inalenga kutatua changamoto ambayo inahitajika ufumbuzi wa haraka kama vile msongamano kwenye maeneo ya umma. Lakini pia lengo lingine la ujenzi huu wa haraka ni kuweza kufikia uhitaji na mradi husika kuanza kuingiza faida mapema na hivyo kuendana na masharti au matakwa ya benki ya kuanza kurudisha mkopo mapema na kumaliza kwa muda muafaka ili kuepuka adhabu za makato zaidi.
Ujenzi huu wa haraka pia hufanyika ikiwa kuna nyumba inatakiwa kuhamiwa haraka sana kwa kuwa wenyewe wahusika wanatakiwa kuwasili mji husika mapema zaidi wakati nyumba yao ikiwa tayari imekamilika. Hivyo kuna wakati uhitaji wa aina hii ya ujenzi wa haraka huwa muhimu sana kulingana na mahitaji yake. Ikiwa unahitaji ujenzi wa haraka wa namna hii unaweza kuwasiliana nasi tukakupatia wahusika.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!