FAIDA ZA UJENZI WA HARAKA(FAST TRACK CONSTRUCTION)

Ujenzi wa haraka huhusisha kazi nyingi kufanyika kwa wakati mmoja ili kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda mfupi uliopangwa. Ikiwa kuna usimamizi sahihi ujenzi huenda vizuri na kwa umakini mkubwa na hivyo malengo kufikiwa na huja na manufaa yake makubwa.

Faida za Ujenzi wa haraka(Fast Track Construction).

UJENZI WA HARAKA UNAKUJA NA MANUFAA MAKUBWA

Kupunguza gharama na kuongeza faida.

Mradi wowote na hasa wa kibiashara unapotumia muda mchache zaidi katika kujengwa husaidia sana kupunguza gharama hasa kwa upande wa gharama za utaalamu. Lakini pia mradi wa jengo la kibiashara unapotumia muda mchache kukamilika maana yake moja kwa moja jengo linaanza kutumika, kuuzwa au kupangishwa na hivyo faida inaanza kupatikana na mapema na kupelekea kuanza mradi mwingine kwa haraka na faida kuzidi kukua.

UJENZI WA HARAKA HUPUNGUZA GHARAMA ZA KITAALAMU NA JENGO KUANZA KUINGIZA FAIDA HARAKA

Mradi kumalizika mapema.

Ujenzi wa haraka hupelekea mradi kumalizika mapema na hivyo kuja na manufaa mengi yanayotakana na mradi kumalizika mapema na kwa muda uliopangwa ikiwemo mkandarasi kuaminiwa zaidi na kukwepa adhabu zinazotokana na kucheleweshwa kwa mradi. Kumalizika hara kwa mradi husaidia hata mikopo kwenye mabenki kulipwa haraka na kuepuka riba kubwa na adhabu mbalimbali katika kurudisha fedha, jambo ambalo huja na manufaa makubwa ya kuokoa fedha ambazo zingeweza kupotea kutokana na mradi kuchelewa.

UJENZI WA HARAKA HUPELEKEA MRADI KUMALIZIKA HARAKA NA KUEPUKA ADHABU ZINAZOTOKANA NA KUCHELEWESHWA KWA MRADI AMBAZO NI SEHEMU YA HASARA YA MRADI AU KUCHELEWESHWA MAREJESHO YA MIKOPO YA BENKI NA KUSABABISHA RIBA KUWA KUBWA

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *