RAMANI NA UJENZI MWANZA
Mwanza ni moja kati majiji ambayo sekta ya ujenzi inakuwa kwa kasi sana Tanzania. Hata hivyo Halmashauri ya jiji la Mwanza na halmashauri ndogo za pembeni ya jiji kama vile Misungwi na Sengerema ni kati ya halmashauri ambazo mamlaka za ujenzi zimekuwa “serious” sana.
Miradi ya ujenzi inayofanyika katika maeneo yanayoonekana iwe ni ndani au nje ya maji hasa katika maeneo yaliyopo karibu na barabara au mji hufuatiliwa kwa karibu sana kuona kama imetimiza imefuata utaratibu uliowekwa na mamlaka husika.
Japo hata hivyo bado kuna miradi mingi ya ujenzi inayofanyika Mwanza bila kufuata utaratibu lakini ni kwa sababu haijashika umakini wa watu wa mamlaka husika.
Mwanza ni jiji lenye gharama kiasi kwenye suala la gharama ya vifaa vya ujenzi na hata ufundi licha ya kwamba ni eneo ambalo halina mafundi wengi wenye uwezo wa juu sana kama ilivyo kwa Dar es Salaam.
Changamoto kubwa ya ujenzi Mwanza ni mawe na miamba migumu ambayo mara nyingi mtu hukutana nayo chini ya ardhi wakati wa kuchimba msingi wa jengo ambapo miamba mingine ni imara na mikubwa sana kiasi kwamba kitaalamu hupelekea kuamua kujenga juu ya mwamba wenyewe.
Karibu kwa ushauri wa ujenzi na msaada wa kitaalamu kwa ujenzi Mwanza
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!