KABLA YA KUPAUA JENGO.
Changamoto kubwa sana tunazokutana nazo kwenye ujenzi huwa zinatuathiri kwa sababu mara nyingi huwa hatuzitegemei kutokea bali zinakuja kwa kama ajali katika wakati ambao pengine tumeshachelewa au tunahitaji kutatua kwa gharama kubwa sana. Na moja kati ya sababu ya changamoto hizo kujitokeza ukiachilia mbali uzembe na ubadhirifu basi huwa ni kukosa ushirikiano kama timu ya ujenzi kuelekea kutimiza maono ya mradi husika hasa kupitia vikao na maridhiano ya mara kwa mara kuhusiana na mambo mbalimbali ya mradi huo. Kukosekana kwa vikao na kushauriana kunakosababishwa na sababu mbalimbali ni tatizo kubwa sana ambalo halionekani kupewa uzito unaostahili.
Sasa nirudi kwenye makala yetu ya inayohusu kabla ya kupaua jengo. Wakati kazi uashi inamalizkia kwenye kujenga zile kuta za mwisho au kama ilivyozeleka kuitwa “kozi za mwisho” za tofali kabla ya gebo na mbao za kenchi inapaswa fundi wa paa afike katika eneo la ujenzi kuangalia michoro inachotaka kwenye kazi yake ya paa na uhalisia wa kazi ambayo imeshafanyika namna inaakisi uhalisia. Mtaalamu wa paa ataangalia nini kinachokosekana na nini kinachotakiwa kufanyia marekebisho ili kumwezesha yeye kufanya kazi yake kwa usahihi na ubora. Baada ya kugundua maeneo yanayotakiwa kuboreshwa ikiwa yapo basi mafundi uashi watapaswa kufanya hivyo au kurekebisha ikiwa walishakosea kabla ya kupisha kazi ya paa kuanza kwa kadiri michoro inavyoelekeza na kwa kadiri ya viwango vilivyokubalika.
Kwa hivyo sasa mtu wa paa anapokuja kufanya kazi yake inakuwa rahisi sana kwani alishahakikisha changamoto zote za kwenye kazi iliyopita nyuma zinazoathiri ubora wa kazi ya paa zimetatuliwa. Hii ni kwa sababu mara nyingi sana kazi ya masonry huwa na matatizo mengi ambayo hupelekea kazi ya paa aidha kuharibika pia au kupoteza muda mwingi na gharama kuifanya na kusababisha hasara na mzigo mkubwa kwa fundi wa paa au msimamizi anayesimama ubora. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kanuni hii kwamba kabla ya kazi ya masonry kumalizikia fundi wa paa anapaswa kuwepo na kuhakikisha kwamba kazi imefanyika vizuri na kwa namna ambayo haitakwamisha kazi yake.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255 717 452 790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!