UNAJUAJE JENGO LAKO LIMEZINGATIA VIGEZO MUHIMU KABLA HUJAWEKA FEDHA? FANYA HIVI.

Siku zote binadamu tunatofautiana sana kwa mambo mengi, japo kwenye maisha tunajikuta tukijihusisha na vitu lakini sio vitu vyote huwa vinateka umakini wetu na sisi kuvipa uzito mkubwa. Kuna vitu vingi sana viko kwenye maisha yetu ambavyo tunajihusisha navyo lakini ni vichache tu ambavyo huwa vinatuvutia kiasi cha kuvipa umakini wetu. Hili limepelekea kwa maeneo yale ambayo yanatuhusu lakini hatuyapi umakini mkubwa kutofanyika maamuzi sahihi au kutopata matokeo bora kwa sababu ya kufanyika ilimradi na wale tuliowaachia.

Sasa kwenye ramani za nyumba zetu hili nalo hujitokeza sana na tofauti na maeneo mengine madhara ya kwenye nyumba huja na gharama kubwa kutokana na uhalisia wa gharama za ujenzi jinsi zilivyo juu sana. Hivyo ikiwa wewe sio mtu ambaye ujenzi huwa unateka makini wako na kupenda kufuatilia basi ni muhimu sana uhakikisha unazingatia mfumo ambao utahakikisha umefanya kazi yenye ubora na iliyozingatia vigezo vyote muhimu kabla ya kuchukua fedha na kuanza kuziweka kwenye mradi wenyewe.

Unachotakiwa kufanya hapa ni kwanza kuhakikisha unafuatilia mambo yote muhimu ya kuzingatia kabla hujatengeneza mchoro wa ramani ambayo nimeyaandika kwenye makala zilizopita unaweza ku-google hapa kwenye ujenzi makini ukajionea kisha baada ya kupitia ukashirikisha pia watu wengine ikiwemo wataalamu na watumiaji wa jengo na kuhakikisha umepata vitu vyote muhimu vya kuzingatia. Kutokea hapo utatengeneza mwongozo ambao ndio utaufuata ambao utakuwa unakuongeza juu ya mambo yote ya kuzingatia wakati unafanya kazi na mtaalamu wako ambaye utamwita baada ya kutengeneza mwongozo huo.

Kisha utamshirikisha mtaalamu huyo mwongozo huo na yeye kuongezea utaalamu wake kutengeneza ramani yenye ubora wa hali ya juu na kisha kuja kuwasilisha kwako ile rasimu ya kwanza ya michoro ya ramani. Kwa pamoja mtaiangalia huku mkizingatia yote yaliyoorodheshwa kwenye mwongozo huo kuhakikisha hamsahau kitu chochote ambacho kiliazimiwa isipokuwa tu kama mtaamua wenyewe kwa hiari yenu kwamba hamkihitaji tena kwa kile mnachotaka kufanikisha kwenye nyumba/jengo hilo.

Kwa kuzingatia hayo mtu utakuwa na uhakika wa kuwa na jengo bora na zuri lililozingatia vigezo vyote ambalo hutakuja kujutia baadaye kwamba kuna vitu ulisahau au hata kuingia gharama nyingine ya kuvunja na kurekebisha ambayo ni hasara ungeweza kuipuka mapema kama ungezingatia kufuata mwongozo uliojiwekea kwa kufuata utaratibu wa mwongozo huo hapo juu. Ikiwa unahitaji ushauri zaidi au huduma nyingine yoyote usisite kuwasiliana nasi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *