MATOKEO BORA KWENYE MRADI WA UJENZI NI MCHANGANYIKO WA UTAALAMU NA UZOEFU.

Mara nyingi watu huwa wanashindwa kuelewa nini kinachofanya mradi wa ujenzi kufanya kwa ubora na kwa viwango vilikusudiwa au hata kuvuka matarajio yaliyokusudiwa kwenye mradi husika. Matokeo bora ya mradi wa ujenzi ni pamoja na ubora wa kazi iliyozingatia vigezo vyote vya ubora na utaalamu sambamba na kukamilika ndani ya muda uliowekwa na ndani ya bajeti ya gharama iliyopitishwa na timu husika ya mradi huo wa ujenzi.

Sasa huwa ni makosa sana kudhani kwamba mtu akishakuwa mtaalamu anaweza kufanikisha mradi wa ujenzi kwa vigezo vyote vilivyokusudia kama hana uzoefu wa miradi iiyopita na kuvuka changamoto zake mbalimbali. Hali kadhalika ni makosa kudhani kwamba mtu mwenye uzoefu kama vile wasimamizi wa ujenzi maarufu kama “foreman” au mafundi wanaweza kufanikisha matokeo bora kwenye mradi pasipokuwa na mwongozo na usimamizi wa mtaalamu au wataalamu wa fani husika.

Mara zote muunganiko wa haya mawili unapokosekana basi mradi mara nyingi huwa na changamoto nyingi za kiufundi au makosa mengi ambayo yanatokana na kukosekana kwa kimojawapo. Hivyo ni muhimu na ni vyema kila mradi wa ujenzi ufanyike chini ya msimamizi mwenye utaalamu na uzoefu kwa pamoja au ashirikiane na wenye uzoefu ili kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa ubora na usahihi sana kwa kuzingatia changomoto na dharura zote zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji.

Jambo la msingi na la kuzingatia sana ni kwamba kwa watu ambao sio wataalamu wanapaswa kila mara kuuliza na kupata maelekezo kutoka kwa mtaalamu kabla hajaendelea mbele na mradi wa ujenzi kwani makosa mengi hutokea kwa sababu ya kukosa au kutofuata maelekezo ya mtaalamu husika wa mradi wa ujenzi. Mtaalamu au wataalamu huona mambo yote ya kitaalamu yapopuuzwa wakati fundi mzoefu huweza kuona changamoto wakati utekelezaji. Lakini unapokutana na mtaalamu ambaye pia ni mzoefu basi mambo yanakwenda vizuri zaidi kwani uongozi wake unakuwa wa uhakika na usio na mashaka yoyote.

Karibu kwa huduma ya ujenzi na ramani za majengo ya aina zote.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *