AINA ZA MADIRISHA KUTOKANA NA MUUNDO.

Inaendelea.

-MADIRISHA YANAYONINGINIA/HUNG/SASH WINDOWS – Hii ni aina ya madirisha ambayo hutembeak ama ilivyo kwa sliding windows lakini tofauti yake ni kwamba hung/sash windows yatembea kutoka juu kwenda chini au chini kwenda juu kama yananinginia. Katika aina hii ya madirisha aina maarufu zaidi ni yale ambayo linafunguka dirisha moja na sehemu nyingine ni sehemu isiyofunguka, japo kuna aina nyingine ambayo yako kwa uchache ambayo panel zote mbili, ya juu nay a chini zinafunguka.

DIRISHA YANAYONINGINIA/HUNG WINDOW

-MADIRISHA YANAYOFUNGUKIA JUU/AWNING WINDOWS – Hii ni aina ya madirisha ambayo bawaba zake ziko upande wa juu wa dirisha na dirisha lenyewe linafungukia upande wa juu na nje ya nyumba. Madirisha haya wakati mwingine huwa na changamoto sana kwenye kuyafungua hasa yanapokuwa mazito kwa maana uzito wake hulazimisha yarudi kujifunga tena.

DIRISHA LINALOFUNGUKIA JUU/AWNING WINDOW

-MADIRISHA YANAYOZUNGUKA/PIVOTING WINDOWS – Hii ni aina ya madirisha ambayo huzunguka katika mhimili wa katikati ulilishikilia dirisha katika kufunguka, ambapo nusu ya paneli ya dirisha huwa ndani ya chumba na nusu nyingine huwa nje pale linapokuwa limezunguka kwa nyuzi 90. Hii ni aina ya madirisha ambayo hutumika mara chache.

DIRISHA LINALOZUNGUKA/PIVOTING WINDOW

MADIRISHA YANAYOTEMBEA, KUJIFUNGA NA KUJIFUNGUA/SLIDING FOLDING WINDOWS – Hii ni aina ya madirisha ambayo hutumika kwenye maeneo yenye uwazi mpana sana. Ni madirisha ambayo yanaweza kufunguka kawaida sambamba na kutembea katika reli yake pia. Madirisha haya huweza kutembea kuelekea upande wowote na kufunguka kawaida pia.

DIRISHA LINALOTEMBEA, KUJIFUNGA NA KUJIFUNGUA

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *