PAA LA VIGAE VYA MBAO
Vigae vya mbao ni aina ya vigae vinavyotengenezwa na aina na vipande vya mbao ambavyo huweza kupendeza sana na kuvutia kila anayelitazama paa.
FAIDA ZA PAA LA VIGAE VYA MBAO.
-Paa la vigae vya mbao hutengeneza uzuri wa asili wa katika jengo unaoleta upekee unaoendana na ubunifu wa jengo lenyewe usioisha kwa miaka mingi ya maisha ya paa lenyewe.
-Paa la vigae vya mbao linadumu muda mrefu hasa maeneo ya joto yasiyo na unyevu, kiasi cha kufikia hata miaka 40 baada ya kuwekwa.
-Paa la vigae vya mbao linaweza kupatikana katika staili na rangi tofauti tofauti kiasi cha kuweza kuendana na kila aina ya ubunifu wa jengo ulipendekezwa na msanifu.
CHANGAMOTO ZA PAA LA VIGAE VYA MBAO
-Paa la vigae vya mbao linahusisha gharama kubwa kidogo ukilinganisha na aina nyingi za vigae japo sio kwa kiasi kikubwa.
-Paa la vigae vya mbao lina hatari kubwa zaidi ya kushambuliwa na wadudu kama vile mchwa kutokana na urahisi wa mbao zenyewe kushambuliwa na wadudu hivyo litahitaji kutumia madawa mengi na kemikali zaidi kulihudumia mara kwa mra ili kujikinga na hatari hizi.
-Paa la vigae vya mbao pia liko kwenye hatari kubwa ikitokea ajali ya moto kwani linashika moto kiurahisi hivyo rahisi kuteketea kwa ajali ya moto.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!