MFUMO WA PAMPU ZA MAJI ZA ZIMAMOTO.

Kwa kawaida pampu za zimamoto huwekwa kwenye chumba maalumu cha pampu karibu sana na stoo ya mapipa ya maji ya kuzima moto. Pampu zinapaswa kukaa chini ya usawa ya mapipa ya maji ya kuzima moto ili maji yote yaweze kusukumwa kiurahisi kutoka kwenye mapipa wakati wa kuzima moto.

Kama ilivyo mifumo mingine kunatakiwa pia kuwe na pampu za dharura ikiwa pampu kuu imepata hitilafu ya aina yoyote na kupelekea kushindwa kufanya kazi. Kunatakiwa kuwepo na pampu kuu ambayo inatumia umeme kisha iwepo pampu nyingine ya dharura ambayo nayo inatumia umeme pia, kisha iwepo pampu nyingine inayotumia mafuta ikiwa umeme umekatika jambo ambalo hutakea mara kadhaa. Pampu zote hizi zinapaswa kuwa na uwezo unaolingana kwamba zinaweza kusukuma maji yote yaliyoko kwenye mapipa wakati wa kuzima moto.

PAMPU YA ZIMAMOTO

Pampu hizi zinaendeshwa na vihisishi(sensors), pale mtaalamu wa kuzimamoto anapofungua zimamoto hydrant au sprinklers zinajifungua zenye pampu zinahisi naa kusukuma maji kwenye nguvu kutoka kwenye mfumo. Sensors za presha zinapohisi tone la maji limeanguka linaruhusu presha kubwa ya kusukuma maji. Lakini kuizima pampu ya maji inahitaji mtalaamu wa zimamoto akazime moja kwa moja kwa kutumia mikono. Huu ni utaratibu uliowekwa kimataifa ili kuzuia pampu zisijizime zenyewe kiholela.

UWEZO WA PAMPU HIZI UNACHANGIWA NA MAMBO YAFUATAYO

-Ukubwa wa eneo ambalo zimewekwa pipa za maji(hydrants)/ au sprinklers

-Idadi ya pipa za zimamoto au sprinklers

-Ukubwa wa eneo ambalo pipa za maji zinazojiwasha zenyewe(sprinklers) zinakaa

-Mpangilio wa ramani ya jengo.

PAMPU YA ZIMAMOTO

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *