JENGO SAHIHI KWAKO NI LILE LINALOENDANA NA UTAMADUNI WAKO NA KUKIDHI MAHITAJI YAKO.

Unaweza kuwa unajiuliza sana kwamba jengo sahihi kwako ni lipi na utajuaje kwamba hilo ndio jengo sahihi na limefikia vigezo vinavyokubalika.

Kwanza kabisa jengo sahihi linapaswa kuzingatia kanuni kadhaa za kitaalamu ambazo zina manufaa kwa maisha ya jengo kiufundi na kimatumizi, kisha liwe limeepuka gharama zisizo za lazima ambazo hazijaridhiwa na mteja.

Jengo sahihi linatakiwa liwe limepitishwa na kukubalika na mamlaka za eneo husika zinazohusika na kukagua na kupitisha sharia zinazosimamua viwango vya majengo.

Muhimu kuliko vyote ni jengo sahihi linapaswa kuwa limekidhi mahitaji ya mteja na kuendana na utamaduni wake kwenye kila nyanja na kukidhi matamanio yake ambayo yatapelekea kuridhiwa na mteja lakini huku likizingatia viwango vilivyowekwa na mamlaka husika.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *