KATIKA MRADI WA UJENZI MTEJA ANAHITAJI MTAALAMU WA KUSIMAMIA MASLAHI YAKE.

Baada ya michoro ya ramani za mradi wa ujenzi kukamilika mteja aidha hutafuta mkandarasi na kumpa kazi ya kujenga mradi husika. Haijalishi ni mkandarasi mkubwa au mkandarasi mdogo au hata fundi wa kawaida wa mtaani ambaye naye anaangukia kwenye kundi hili la ukandarasi.

MSHAURI WA KITAALAMU

Hata hivyo licha ya kwamba mteja anaweza kumuamini sana huyu mkandarasi kwenye utekelezaji wa mradi huu kwa uaminifu na kwa uhakika mkubwa lakini bado atahitaji mtaalamu ambaye atakuwa anaufuatilia mradi kwa karibu sana kulinda maslahi ya mteja. Kwa vyovyote vile mkandarasi ni mtu mwenye mtazamo wake binafsi tofauti na hata malengo na nia inayoweza kuwa tofauti na mteja katika mradi husika, hivyo katika kutekeleza mradi anaweza aidha kwa kumshawishi mteja au kwa kujiamulia mwenyewe kufanya mambo ambayo hayana manufaa kwa mradi wala kwa mteja wa mradi husika.

MSHAURI WA KITAALAMU ANA KAZI YA KUSIMAMIA MASLAHI YA MTEJA KATIKA MRADI WA UJENZI

Hivyo kuwepo kwa mtaalamu wa ujenzi kwa maana ya msanifu majengo mzoefu au pamoja na mhandisi mihimili endapo mradi ni mkubwa sana kutasaidia kuchunguza kila maamuzi anayofanya mkandarasi na kumshauri kwa usahihi mteja ambapo kazi kubwa ya mtaalamu wa ushauri itakuwa ni kulinda maslahi ya mteja. Kwa utaratibu huu mteja atakuwa kwenye nafasi ya kujihakikishia kwa maba maslahi yake yanalindwa na kazi inafanyika kadiri ya malengo yake na malengo ya mradi wenyewe husika. Mteja ataongeza thamani kubwa ya mradi wake au jengo lake kupitia huduma hii.

MSHAURI WA KITAALAMU ANAYESIMAMIA MASLAHI YA MTEJA ATAONGEZA THAMANI KUBWA KWENYE MRADI HUSIKA

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *