EPUKA RAMANI ZA KWENYE MITANDAO, KUTANA NA MTAALAMU.
Kabla kufikiria kuchukua ramani ya kwenye mtandao kwanza anza kufikiria ikiwa ramani husika itakuwa na changamoto au katikati ya ujenzi ukabadili mawazo na kutaka kufanya marekebisho kidogo ya ramani kabla hujaendelea, ni nani atakayekufanyia kazi hiyo ya kitaalamu?
Kazi za kutoa huduma za kitaalamu ni tofauti kidogo na biashara za kuuza bidhaa ambapo ukishainunua unaweza kuanza kuitumia hapo hapo na kuona kama iko sawa au ina changamoto yoyote, kwenye huduma za kitaalamu kwa mfano ujenzi kazi haiishi baada ya kukabidhiwa michoro ya ramani bali kazi ndio kama inaanza baada ya ujenzi kuanza. Kwa kawaida hutokea changamoto nyingi na mabadiliko ni kitu ambacho hutokea mara zote ambapo mabadiliko mengine huwa makubwa kiasi cha kulazimu mtaalamu husika kuingilia na kuangalia changamoto husika na kutoa ushauri wa kuhusu nini kifanyike.
Kama ramani umenunua mtandaoni na ilipofika katika uhalisia mambo yakaenda tofauti na matarajio ikalazimu ibadilishwe hiyo ina maana kwamba ni aidha utakubaliana na makosa hayo kwa sababu huna namna au utalazimika kutafuta mtaalamu mwingine ambaye ataanza upya kupambana na kazi hiyo na hivyo itakugharimu zaidi sambamba na usumbufu itakaoambatana nao, vitu ambavyo hukuvitegemea kabla. Hivyo ili kuondokana na usumbufu wote huu epuka kabisa kuchukua au kununua ramani za mitandaoni na badala yake tafuta mtaalamu mtakayeonana ana kwa ana na kushirikiana kutengeneza ramani ya nyumba yako inayoendana na uhalisia wa kimazingira na inayotokana na mawazo yako moja kwa moja.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!