RAMANI ZA KWENYE MITANDAO HAZIKIDHI VIGEZO VYA KIMAMLAKA.

Kama tulivyotangulia kukubaliana kwenye makala zilizopita kwamba ramani za kwenye mitandao hazizingatia vigezo vya kiwanja ili kuja na aina sahihi ya ramani inayoendana na kiwanja husika. Hali kadhalika mamlaka husika huweka vigezo vingi ambavyo michoro inapaswa kukidhi ili uweze kupatia kibali na kuruhusiwa kujenga eneo husika, vigezo ambavyo mara nyingine hutofautiana kati ya eneo moja na jingine kwa sababu nyingi mbalimbali ambazo hata wataalamu wenyewe mara huhitajika kufuatilia ili kuwa na uhakika kamili wa vigezo husika na sababu zake.

NI VIGUMU KUJUA VIGEZO VILIVYOWEKWA NA MAMLAKA ZA UJENZI KWANI HUTOFAUTIANA ENEO MOJA NA JINGINE

Ramani za kwenye mitandao hazifanyiki kufuatana na vigezo vilivyowekwa na mamlaka husika kwa sababu licha ya kwamba hazizingatii hata asili na ukubwa wa eneo husika la ujenzi lakini pia hawawezi kufahamu haswa ni vigezo gani vinahitajika na mamlaka husika. Lakini hata kama ikatokea wamejua vigezo vya mamlaka ya eneo fulani, labda halmashauri ya manispaa fulani bado kila eneo na kila mamlaka ina vigezo vinavyotofautiana, na vigezo hivi pia hubadilika baada ya muda. Hivyo inakuwa vigumu zaidi kwa ramani za mitandaoni kukidhi vigezo vya kimamlaka linapokuja suala la ramani za ujenzi.

UTAJIKUTA UNALIPIA GHARAMA MARA MBILI ILI KUWEZA KUKIDHI VIGEZO VILIVYOWEKWA NA MAMLAKA YA ENEO HUSIKA UNAPOJENGA

Kwa bahati mbaya zaidi unaponunua ramani ya mtandaoni na kukuta kwamba haikidhi vigezo vya kimamlaka ya eneo husika unapojenga unatakiwa kuibadilisha iweze kuendana na vigezo vinavyohitajika, ambapo hapa sasa ndipo utakapohitaji tena mtaalamu wa kukufanyia mabadiliko ambaye atakuwa kama anaanza upya kufanya kazi hiyo kwa sababu hajui ilipotokea au ilipoanzia na hivyo unakuwa kwenye upande wa hasara kwani unajikuta ukilipia gharama mara mbili.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *