KUJENGA NYUMBA YA GHOROFA YA KISASA KWA MALIGHAFI ZENYE UBORA.
Tofauti kati ya gharama ya nyumba iliyojengwa kwa malighafi zenye ubora ule ambao uko kwenye viwango vinavyokubalika na nyumba iliyojengwa kwa malighafi feki au za viwango vya chini kwa kawaida huwa sio kubwa sana, lakini madhara yanayotokana na ujenzi wa jengo lililojengwa kwa malighafi feki au za viwango vya chini ni kubwa sana na huwa haichukui muda mrefu kabla hujaanza kuona matokeo yake.
Ni muhimu sana katika ujenzi mtu ufikirie mara mbili kabla ya kuamua kununua malighafi zisizo na ubora kwa kisingizio cha bei, hiyo bei unayoiona ni ghali itakuja kuonekana ni nafuu sana siku za usoni pale ambapo utajikuta kwenye majuto makubwa huku ukitakiwa kununua upya malighafi zenye ubora kwa gharama ile ile uliyoikimbia. Nashauri kwamba mtu usikimbilia rahisi bila kujiridhisha na ubora wake kwani tunavyoongea hapa tumeshakutana na kesi nyingi sana za matengenezo upya yaliyopelekea kuingia gharama kubwa nyingine kwa utumiaji wa malighafi zilizo chini ya kiwango.
Kuwa na amani pamoja na Imani na jengo lako kwa kulipenda kwa kuhakikisha unafanya kazi ya uhakika kwa kufanya maamuzi sahihi ya kununua vyenye ubora.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!