UJENZI WA GHARAMA NAFUU KWA KUJENGA KWA AWAMU.

Kila njia ambayo unaweza kujaribu kuitumia katika kupunguza gharama za ujenzi ina faida zake na changamoto zake japo kuna nyingine zina faida kubwa zaidi kwa baadaye kwa mtu mvumilivu kuliko nyingine. Njia ya kutafuta unafuu wa gharama za ujenzi kupitia kujenga kwa awamu ni kati ya njia hizi muhimu na zenye faida zaidi kwa mtu mvumilivu kuliko nyinginezo, kwa sababu kwa njia hii mtu hapunguzi chochote bali anatengeneza michoro ya ramani ya viwango anavyovitaka bila kupunguza chochote au kulazimika kujenga asichokitaka na badala anafanya vile atakavyo.

UNAFUU WA GHARAMA KWA KUJENGA KWA AWAMU KUNAKUSAIDIA KUFIKIA NDOTO YAKO BILA KUTISHWA NA GHARAMA

Lakini anakuwa na mpango sahihi wa namna ya kujiandaa kuhamia jengo husika kabla hajakamilisha maeneo yote huku akiendelea kukamilisha eneo moja baada ya jingine na kulihamia. Kwanza inataka uvumilivu wakati wa kuanza kujenga ambapo mtu unakuwa huna haraka wala papara katika kufanya mradi wako bali unazingatia mambo yote muhimu na mahitaji yako yote katika mradi husika. Kisha baada ya hapo kwa ushauri wa mtaalamu anayefanya kazi husika mnapanga mtaanza kukamilisha wapi na kuhamia bila kupata usumbufu mkubwa wakati maeneo mengine yakiendelea kukamilishwa taratibu, kwa njia hii mtu anaweza kuendelea mpaka anakamilisha jengo lake kwa uhakika, kwa ubora na kwa ukubwa anaouhitaji.

MPANGILIO SAHIHI WA UJENZI WA AWAMU UTAKUPUNGUZIA USUMBUFU WAKATI WA KUJENGA HUKU UKIKUPATIA HUDUMA BORA SANA

Kujenga kwa awamu inaweza kukuchukua muda mrefu mradi kukamilika, wakati mwigine hata miaka kadhaa lakini ni njia nzuri ya kufanya uchaguzi sahihi na utakaoufarahia zaidi nap engine utakuondolea hasara na usumbufu wa kuja kufikiria kujenga tena wakati umepata pesa zaidi na kuona nyumba yako ya mwanzo uliyoijenga kwa haraka ikiwa inakubana au haina hadhi ambayo utakuwa unafikiri umeifikia kwa wakati huo.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *