GHARAMA ZA VIBALI VYA UJENZI ZINABADILIKA

Kama tulivyozungumza awali vibali vya ujenzi vimegawanyika katika makundi mawili makubwa kwa mtu ambaye hayuko kwenye sekta ya ujenzi. Kuna vibali vinavyotolewa na halmashauri za jiji, manispaa au miji ambazo ndio huitwa vibali vya ujenzi na kuna vile vinavyotolewa na bodi za ujenzi kwa mfumo wa stika za ujenzi. Kibali cha ujenzi kutoka halmashauri ya jiji, manispaa au mji ndio huweza kuwa na changamoto kidogo kwenye kukipata kwa sababu kwanza ndio kibali cha kwanza ambacho ahata bodi zenyewe za ujenzi wanategemea kukitumia ili kukupa ruhusa ya kuendelea na ujenzi lakini pia ndio kibali kinachopitia kwenye idara zote muhimu za halmashauri ya jiji, mji au manispaa kama vile idara ya mipango miji, idara ya mazingira, idara ya afya, ujenzi n.k. ili kukaguliwa kama mradi husika umetimiza vigezo na masharti ya kupewa kibali. Baada ya kuwa na kibali cha ujenzi kutoka halmashauri ya jiji, manispaa au mji husika kupata vibali vya kwenye bodi za ujenzi kama vile bodi ya wasanifu majengo na wakadiriaji majenzi, bodi ya wahandisi na bodi ya wakandarasi sio tena kazi ngumu wala haichukui muda lakini gharama yake kwa ujumla ni kubwa kuliko gharama ya kibali cha ujenzi kutoka halmashauri husika.

BODI ZA UJENZI

Hata hivyo gharama za vibali vya ujenzi kutoka halmashauri za majiji, manispaa na miji zimeongezeka sana miaka ya hivi karibuni na kwa kasi kubwa sana kiasi cha kuzidi gharama ya stika moja ya bodi ya ujenzi. Hasa miaka ya hivi karibuni watu wamekuwa wakishangaa ukubwa wa gharama japo hawajui zilikuwa kiasi gani miaka michache iliyopita. Kufikia mwaka 2015 gharama za kupata kibali cha ujenzi wa nyumba ya ghorofa moja ilikuwa ni wastani wa Tshs 90,000 au pungufu ya hapo, lakini ilipofika mwaka 2016 gharama hizi ziliongezeka kufikia wastani wa Tshs 150,000 ambapo bado zilikuwa zinaonekana ni kidogo sana ukilinganisha na gharama za vibali vya kwenye bodi za ujenzi zinazotolewa kwa mfumo wa stika. Hata hivyo kufikia mwaka 2019 gharama za kupata kibali cha wastani wa jengo la ghorofa moja zimepanda tena kwa kiwango kikubwa sana kufikia Tshs 700,000 au zaidi kwa wastani. Hii imepelekea gharama za kuoata kibali cha ujenzi wa jengo la ghorofa moja kufikia na kuzidi gharama za kupata kibali cha kutoka bodi yoyote ya ujenzi kwa wastani kinachotolewa kwa mfumo wa stika. Hata hivyo licha ya gharama za vibali vya ujenzi kutoka halmashauri za majiji, manispaa na miji kuongezeka kwa takriban asilimia 700% gharama za stika za ujenzi kutoka kwenye bodi za ujenzi ambazo zilikuwa juu sana zimeongezeka kwa kiasi kidogo sana.

GHARAMA ZA VIBALI VYA UJENZI KUTOKA HALMASHAURI ZIMEONGEZEKA SANA

Ujenzi wa nyumba isiyo ya ghorofa na ambayo sio kubwa sana au yenye utata kwa upande wa mihimili inahitaji kinali cha ujenzi kutoka halmashauri ya jiji, manispaa au mji husika peke yake. Vibali vya ujenzi kutoka kwenye bodi za ujenzi ni kwa majengo ya ghorofa pekee au majengo makubwa yenye mihimili ya mifumo tata.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *