USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 15 UJENZI WA HEKALU
KITABU: FOUNTAINHEAD.
AUTHOR: AYN RAND.
1. Ellsworth Toohey anamwambia Dominique kwamba yeye ndiye aliyempendekeza Howard Roark kwa Hopton Stoddard. Ellsworth Toohey anasema ana lengo la kumfanya Howard Roark kuwa maarufu.
2. Wanajadili ni kwa nini Howard Roark ameamua kumpa Steven Mallory kazi ya kuchonga sanamu. Kisha wanajiuliza pia kwa nini Steven Mallory aliamua kumpiga risasi Ellsworth Toohey, wote hawajui kisha wanasema labda Howard Roark atakuwa anajua sababu.
3. Siku ya uzinduzi wa hekalu la Hopton Stoddard unatangazwa rasmi kuwa itakuwa ni siku ya Tarehe 1, Novemba. Jengo hilo linapata umaarufu na tukio hilo linapata umaarufu mkubwa kupitia kutangazwa na kupambwa sana na vyombo vya habari. Watu wanamzungumzia sana Howard Roark na kuzungumzia sana matarajio yao makubwa kwa hekalu hilo kwa shauku kubwa.
4. Siku ya tarehe 31/Oktoba Hopton Stoddard anarudi kutoka kwenye safari yake ya kidini maeneo mbalimbali duniani. Moja kwa moja anakutana na Ellsworth Toohey ana wanazungumza kwa kirefu.
5. Asubuhi ya tarehe 1/Novemba Hopton Stoddard anatoa taarifa kwamba hakutakuwa na uzinduzi wowote siku hiyo. Hakuna ufafanuzi wowote wa ziada unatolewa.
6. Kesho yake siku ya tarehe 2/Novemba Ellsworth Toohey anaandika kwenye kurasa za makala zake kwamba kuna mengi ya kuzungumzia juu ya mtu anayeitwa Howard Roark, japo ni mtu asiye na umuhimu wowote mkubwa zaidi ya kwamba ameanzisha ujenzi wa jengo lililoshindwa kukamilika.
7. Ellsworth Toohey anaandika kwamba Howard Roark ambaye wengi wenu hamjawahi kumsikia na pengine hamtamsikia tena kuanzia sasa ni Msanifu Majengo. Mwaka mmoja uliopita alipewa jukumu kubwa. Alipewa kazi ya kujenga jengo muhimu sana la kumbukumbu katika jiji la New York, bila uwepo wa mmiliki wake aliyempa uhuru wa kufanya anavyoweza.
8. Ellsworth Toohey anaendelea kuandika kwamba Mr. Hopton Stoddard alikusudia kujitolea kama zawadi kujengwa kwa hekalu la kidini litakalokuwa kama alama ya kiroho kwa imani za watu katika jiji la New York lakini alichokifanya Howard Roark ni ku-design “Godown” (Bohari) japo katika uhalisia haliwezi kuwa Godown bali ni “Danguro” kwa namna linavyoweza kuwakilishwa na sanamu zilizopo. Lakini hili kwa hakika haliwezi kuwa hekalu.
9. Ellsworth Toohey anaendelea kulikosoa zaidi jengo hilo kwa kukosoa muundo wake na vipengele mbalimbali vinavyolitambulisha jengo hilo na kutaja ni namna gani halistahili kabisa kuwa hekalu wala haliendani na hekalu la watu kufanyia ibada. Ellsworth Toohey anaendelea kulikosoa zaidi na kuonyesha kwamba jengo hilo limefika mbali kiasi cha kutukana imani za watu.
10. Siku ya tarehe 3/Novemba Hopton Stoddard anafungua kesi mahakamani kumshtaki Howard Roark kwa kukiuka makubaliano na kutakuwa kulipa fidia ya kurekebisha jengo hilo litakalofanywa na Msanifu Majengo mwingine.
11. Hopton Stoddard akiwa ametoka kwenye safari ya kidini maeneo mbalimbali duniani huku akijihisi mwenye hatia sana kwani hana usafi utakaomuepusha na jehanamu ya moto kwa viwango vya dini zote alizotembelea. Wanaenda na Ellsworth Toohey kutembelea hekalu lake lakini anapoliangalia anaona kwamba halifanani na aina nyingine yoyote ya majengo ya dini aliyotembelea dunia nzima.
12. Anamwambia Ellsworth Toohey kwamba yeye ndiye aliyemwambia kwamba Howard Roark ni Msanifu Majengo mzuri, Toohey anamjibu ni kweli alitegemea afanye kazi nzuri lakini haelewi ni kitu gani kilichotokea.
13. Ellsworth Toohey anamshawishi Hopton Stoddard kwamba makosa yatakuwa yako upande wake. Anamwambia haikuwa sahihi yeye kujenga hekalu kwani hana usafi wa kiroho wa kutosha kujenga hekalu moja kwa moja alipaswa kuanza na vitu vidogo kwanza. Toohey anamwambia hawezi kusamehewa dhambi zake kwa kujenga hekalu kwani hilo linahitaji utakatifu wa hali ya juu, na kwamba jengo hilo halikukusudiwa kuwa hekalu hivyo waligeuze kuwa jengo la kusaidia watu maalum. Walifanye kuwa taasisi ya watoto wenye matatizo maalum.
14. Kesho yake andiko la Ellsworth Toohey lilienda kwenye vyombo vya habari, ambapo jambo lote lilipata umaarufu mkubwa. Watu wengi walipata hasira sana juu ya jengo hilo na wengi walichukia sana kwamba dini imedhihakiwa. Japo hasira juu ya hekalu hilo ilishangaza kila mtu isipokuwa Ellsworth Toohey.
15. Wahubiri wengi makanisa walilihukumu hekalu hilo katika ibada, klabu ya wanawake ikapitisha maazimia ya kufanya maandamano kupinga hekalu hilo, umoja wa wamama ukaandikia waraka wa kupinga hekalu hilo ili kulinda watoto wao dhidi ya maadili mabaya. Msanii mkubwa wa kike aliyetembea maeneo mengine mengi yenye mahekalu akaandika makala inayokosoa hekalu hilo na professor wa chuo kikuu akaandika barua kwa mhariri kukosoa hekalu hilo kadiri ya elimu yake na uzoefu wake. Kiki Holcombe naye akafanya hivyo.
16. Taasisi inayosimamia taaluma ya Usanifu Majengo Marekani ikatoa waraka unaotangaza rasmi kwamba hekalu hilo ni utapeli wa kiroho na kitaalamu. Chama cha umoja wa Wasanifu majengo nao wakaandika barua kuelezea jinsi hekalu hilo linaidhalilisha taaluma ya Usanifu Majengo.
17. Howard Roark mwenyewe hakufanya chochote. Lakini waandishi wa habari walivyomfuata ofisini kwake na kumtaka azungumza lolote juu ya yote yanayosemwa kuhusu hekalu hilo aliwaambia. Yeye hawezi kulazimisha mawazo yake kwenye akili ya mtu yeyote lakini anashauri kwamba kila mtu mwenye kujali aende mwenyewe akalitazame jengo lile kisha atoe maoni yake mwenyewe yanayotoka kwenye mtazamo wake mwenyewe kama atajali kuhusu kuzungumza chochote.
18. Hata hivyo kesho yake habari iliandikwa kwenye gazeti la The Banner kwamba, “Howard Roark ambaye anaonekana anapenda sana kuzungumziwa amepokea kundi la waandishi wa habari ofisini kwake, hakutaka kuongelea chochote juu ya yanayoendelea lakini anachojali yeye ni watu wengi zaidi waone jengo lake”.
19. Howard Roark anakataa kutumia mwanasheria kwenye kesi hiyo, Austen Heller anapingana naye na kumuuliza anawezaje kushinda bila mwanasheria, Howard Roark anamwambia Hopton Stoddard atashinda kesi hiyo na ataamua afanye nini na jengo lake. Austen Heller anamwambia lakini akishinda atatumia hela zake kulirekebisha, Howard Roark anakubali kwamba ni kweli huenda akatakiwa kumlipa fidia hivyo atatumia hela zake.
20. Austen Heller anajaribu kuandika makala kwa hasira sana kumtetea Howard Roark lakini haipati umaarufu wowote na inaishia juu juu.
21. Dominique anamtembelea Ellsworth Toohey ofisini kwake, wanazungumza. Ellsworth Toohey anamwambia Dominique awe shahidi upande wa mlalamikaji na Dominique anamwambia ndivyo alivyopanga lakini anakataa kupangiwa cha kwenda kuongea mahakamani.
22. Kesi kati ya Hopton Stoddard dhidi ya Howard Roark inatangazwa kusomwa mwezi Februari/1931. Hopton Stoddard hahudhurii mahakamani bali anawakilishwa na mwanasheria wake.
23. Ellsworth Toohey ndiye shahidi namba moja upande wa mlalamikaji.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!