USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 24 MIRADI ZAIDI YA UJENZI
KITABU: *FOUNTAINHEAD*
AUTHOR: *AYN RAND.*
1. Dominique na Gail Wynand wanakwenda tena mapumzikoni, na wanajadili mambo mbalimbali ikiwemo siasa kwa kirefu sana.
2. Dominique anajaribu kumshawishi Gail Wynand kumfukuza kazi Ellsworth Toohey kwa sababu ni mtu hatari sana. Dominique anasema ni vyema akamfukuza Gail Wynand mapema kabla hajachelewa.
3. Gail Wynand anapuuzia na kumwambia Dominique kwamba Ellsworth Toohey hawezi kuwa ni hatari yoyote na pia ni mtu mdogo sana kwake. Pia hawezi kumfukuza kwa sababu anamwingizia pesa nyingi sana kwa kuandika makala zenye ushawishi mkubwa. Dominique anamwambia Gail Wynand hajui kwa nini ameamua kuwa mzalendo sana kwake lakini anamwonya kuhusu Ellsworth Toohey.
4. Howard Roark anapewa kazi ya mradi wa Monadnock kama nyumba au hoteli za mapumzikoni zinazolenga watu wa kipato cha kati. Anapewa mradi huo na Bwana Caleb Bradley ambao anaujenga huko Florida.
5. Howard Roark na Steven Mallory wanafanya kazi hiyo ambapo Steven Mallory anachonga sanamu zote muhimu kwenye mradi huo wa Monadnock. Howard Roark anapanga kuchukua nyumba mojawapo kwa mapumziko lakini kabla ya kufanya hivyo anapata ujumbe kutoka New York.
6. Kent Lansing anawasiliana na Howard Roark kumwambia arudi New York kumalizia mradi wa Aquitania hotel baada ya kuendesha kesi kwa miaka mitano na sasa Kent Lansing amebaki peke yake mwenye maamuzi kwenye kampuni.
7. Howard Roark anarudi New York kumalizia mradi wa Aquitania. Kisha anafanya kazi nyingine kadhaa baada ya hiyo. Anajenga nyumba mbili za kuishi huko Connecticut, ukumbi mmoja wa sinema huko Chicago na hoteli moja huko Philadelphia.
8. Wanachaguliwa wasanifu wa majengo 8 ambao watashirikiana kujenga jengo moja kubwa kidunia la World Fear akiwemo Howard Roark, Gordon L. Prescott, Ralstone Holcombe, Peter Keating na wengineo. Howard Roark anakataa kufanya kazi na watu wengi na wengine wote pia wanagoma kufanya kazi na Howard Roark akiwemo Peter Keating. Peter Keating anachukua jukumu la kuwa kiongozi wa timu hiyo ambapo wanaitwa Peter Keating na washirika wake, Howard Roark anaondolewa.
9. Gail Wynand anaagiza Howard Roark aitwe ofisini kwake kwa ajili ya kazi. Hawajawahi kukutana wala kuzungumza lakini Howard Roark anakubali wito na kufika ofisini kwa Gail Wynand.
10. Baada ya kuzungumza kwa kirefu sana Gail Wynand anampa Howard Roark kazi ya kumjengea nyumba nzuri ya kuishi yeye na mke wake nje kidogo ya mji. Howard Roark anakubali lakini kwa masharti ya kutobadilisha chochote kwenye michoro halisi na Gail Wynand anakubaliana naye.
11. Wanaenda kutembelea eneo la ujenzi pamoja huko wanazungumza mambo mengi hususan falsafa kwa kirefu sana.
12. Howard Roark anakamilisha kazi ya michoro ya nyumba ya Gail Wynand inakuwa imebakia kuanza ujenzi. Gail Wynand anajaribu kumwambia kwamba anataka kumpa mkataba wa kujenga nyumba hiyo na mkataba wa kujenga majengo yake mengine yote yanayokuja lakini kwa masharti ya kwamba afuate maoni ya watu.
13. Howard Roark anamkubalia na kisha kumtengenezea mchoro wa haraka haraka hapo hapo kwa mitindo iliyozoeleka na kumwambia kama ndicho anachotaka. Gail Wynand anamwambia hapana, kisha Roark anamwambia basi asirudie tena kumwambia habari za kukubalika na watu.
14. Gail Wynand anacheka sana na kumwambia angeshangaa sana kwa yeye kukubaliana na hilo.
15. Gail Wynand anamwambia Howard Roark anahitaji kula nao chakula cha jioni pamoja ili aweze pia kuonana na mke wake kwani anatamani sana aonane na mke wake. Howard Roark anakubali.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!