MAAMUZI SAHIHI KWENYE UJENZI YANAHITAJI UKOMAVU WA KIAKILI TUNAOUITA BUSARA.

Katika zama za zamani za Misri, Ugiriki na Roma kulikuwa hakuna utofauti unaoelezeka kwa usahihi kati ya maneno busara na usomi. Mara nyingi usomi uliitwa au kufananishwa neno busara kama linavyofahamika katika nyakati za sasa. Pengine hili lilitokana na kwamba watu wengi waliojihangaisha kusoma katika nyakati za zamani walikuwa ni wale waliokuwa na busara kubwa sana ya kimaamuzi na hivyo wengi wao wakatokea kuwa ni watu wenye busara zaidi ukilinganisha na leo hii ambapo kila mtu anasoma na wengi wanafika ngazi za juu kabisa za elimu.

Kwa miaka ya zamani pengine hilo halikuwa tatizo kwa sababu wengi waliojihangaisha kusoma ambapo elimu ilikuwa ni hiyari tena ni kama anasa wasomi wengi walikuwa na busara kubwa na ndio waliokuwa wenye busara katika jamii. Lakini leo hii wote tunajua wazi kwamba busara na elimu ni vitu tofauti kabisa kiasi kwamba hata mtoto mdogo anaweza kutofautisha. Hili kwa sehemu fulani limekuwa ni tatizo kwani wenye elimu kwa kuheshimiwa elimu zao wamepewa nafasi kubwa kimaamuzi lakini kwa sababu baadhi wanakosa busara wakati mwingine hupelekea majinga.

A young black man is a project manager at a residential construction site.

Hata hivyo kwa kulinganisha na wati wengine bado sehemu kubwa ya wasomi kwa wastani wana busara zaidi kimaamuzi ukilinganisha na watu ambao wameishia kwenye ngazi za chini za kielimu. Pengine hili linatokana na mifumo waliyopitia na tabia zilizojijenga kwao au ile hali ya kuaminiwa na kujiamini, kutegemewa na kuwajibika kwa yale wanayokwenda kufanya. Hili limekuwa linaonekana kuanzia kwenye maeneo ya kazi, kwenye malezi ya watoto na machaguo mengine mengi ya katika maisha na ndio maana mtu anapokuwa amefika kwenye ngazi za juu za elimu halafu akafanya mambo ya hovyo watu humshangaa sana na kuona hilo linawezekanaje ukilinganisha na walioishia kwenye ngazi za juu za elimu.

Kwenye miradi ya ujenzi napo jambo hili halijatuacha salama sana, kwa sababu licha ya kwamba kuna watu wengi walioishi katika ngazi za chini za elimu na bado wanafanya maamuzi bora kwenye miradi ya ujenzi lakini ukilinganisha bado utakuta wale waliofikia ngazi za juu za elimu wana nafasi kubwa zaidi ya kufanya maamuzi sahihi na bora kuliko kinyume chake. Na hapo ndipo suala la busara linapoingia kwani hili sio kwa maamuzi ya kiufundi pekee bali mpaka maamuzi ya usimamizi wa ujenzi, usimamizi wa fedha na mengine yote. Msimamizi anapokuwa ni mtu mwenye uzoefu na mwenye uwezo mkubwa kitaaluma basi nafasi ya kufanya maamuzi sahihi na yenye ubora inakuwa ni kubwa sana.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *