NAMNA YA KUJENGA BARABARA YA ZEGE.


1. Hatua za awali za maandalizi ya Barabara yenyewe (Site Preparation)

  • Kuchunguza aina na hali ya udongo wa eneo husika: Lazima kuangalia aina ya udongo kwani ina madhara makubwa kwa ujenzi unaoenda kufanyika eneo husika sambamba na hali ya eneo hilo kama ina mifereji au vyanzo vya maji vinavyoweza kuleta uharibifu.
  • Kuondoa udongo wa juu na vilivyomo vingine juu ya ardhi: Hapa unapaswa kuondoa mimea kama nyasi na miti, mawe, na udongo wa juu (topsoil) ili kuandaa eneo kwa ujenzi kuanza.
  • Kutengeneza msawazo wa ardhi husika: Kuchima na kujaza ili kupata ule msawazo(level) iliyokusudiwa kwenye michoro au kuamuliwakitaalamu kwamba ndio msingi wa Barabara husika utaanzia.

2. Kuweka Tabaka la Msingi la Barabara husika.

  • Kwanza ule udongo wa kwenye msingi iwe utaletwa kutoka sehemu nyingine au utachukuliwa eneo hilo hilo unapaswa kushindiliwa kikamilifu ili usiporomoke zaidi katika kuendelea kumudu matabaka ya juu zaidi ambayo kwa Pamoja ndio yatabeba mzigo.
  • Kuweka tabaka la msingi mfanano wa blinding: Hapa linawekwa tabaka la msingi katika kuendelea na matabaka ya Barabara husika. Tabaka hili linakuwa ni la mawe yaliyoshindiliwa vizuri kwa ujazo wa kati ya inchi sita mpaka kumi na mbili au 150m – 300m.
  • Baada yah apo tutaweka tena tabaka linguine: Hili linakuwa ni tabaka lingine la pili la changarawe au miamba/mawe yaliyovunjwa vunjwa kuongeza uimara wa barabara.

3. Kazi ya useremala ya kutengeneza muundo(formwork).

  • Kutengeneza na kuweka fomu ambayo mara nyingi ni kazi ya mbao au bati kwenye kingo: Hapa unatumia mbao/vibao maalum kama (marine boards) au vyuma kuunda mipaka ya barabara na kuhakikisha unene wa zege unazingatiwa.
  • Kuimarisha zege lenyewe la barabara (Reinforcement): Hapa  tunatumia wavu wa chuma (steel mesh) au nondo (rebar) ili kuongeza uimara wa zege hasa kwenye maeneo yenye mizigo mikubwa kadiri ya michoro inavyohitaji au maelekezo ya mtaalamu aliyetengeneza ramani.

4. Kuchanganya na kumwaga zege (Concrete Mixing & Casting)

  • Kuchanganya zege: Hapa tunatumia mchanganyiko wa saruji, mchanga, kokoto, na maji kwa uwiano sahihi (kwa mfano: 2:4:8 kwa saruji, mchanga na kokoto).
  • Kumwaga zege yenyewe: Hapa tunamimina zege kwenye eneo lililotayarishwa na kuhakikisha inasambazwa sawasawa na kwa msawazo sahihi.
  • Kushindilia vizuri chini kwa kutumia mashine ya kushindilia inayojulikana kitaalamu kama (vibrator): Ili kuondoa nafasi ndani ya zege na kuhakikisha inashikana vizuri na kuwa na uimara wa kutosha.

5. Kusawazisha na kuweka mitaro au chaneli za kupeleka maji sehemu sahihi.

  • Kusawazisha (levelling): Tunatumia vifaa maalum vya kusawazisha kuhakikisha zege inakuwa katika usawazo sahihi na kuwa na uso laini kadiri inavyotakiwa.
  • Kisha tunakata viunganishi ili kuruhusu zege kuwa huru kutanuka na kusinyaa: Hapa ni baada ya masaa machache ya kumwaga zege na kusawazisha, tunakata sehemu ndogo kwenye zege ili kuruhusu kutanuka na kuzuia nyufa zisizotarajiwa zinazoweza kusababishwa na mivutano au kutanuka na kusinyaa kwa zege.

6. Kumwagilia zege yenyewe wakati inaendelea kukauka na kuimarika (Curing)

  • Kufunika na kuimarisha: Wakati wa zoezi hili tumia plastiki au majani ya aina mbalimbali ili kuzuia upotevu wa unyevu unaolowesha zege hilo.
  • Wakati wa kumwagilia maji: Huu ni wakati wa kulowesha uso wa zege kwa siku 7-14 ili kuzuia nyufa za zege na kuhakikisha zege linakuwa na uimara wa kutosha.
  • Muda wa kukaa kusubiri ni kuacha barabara ipumzike: Hapa unazuia vyombo vyote vizito hususan magari kupita kwa angalau siku 14-28 hadi zege liwe na uimara wa kutosha.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *