Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Mabati au Vigae Vya Kupaulia.

  • Hali ya Hewa Ya Eneo Husika:
    Kulingana na mazingira ya eneo lako; maeneo yenye mvua nyingi na upepo mkali unaweza kuhitaji bati imara kama zile zaidi, wakati maeneo yenye jua kali unaweza kutumia tu zisizo na joto kali kama vile vigae vya udongo au vigae vya harvey tiles.
  • Uwezo wa kifedha au Bajeti:
    Ikiwa uwezo wako ni mkubwa unaweza kuchagua aina mbali mbali za vigae bora sana vinavyouzwa kwa hadhi tofauti tofauti lakini kama una uwezo wa kawaida unaweza kuchagua bati nzito zenye muonekano mzuri hata kama wa kigae pia au mionekano ya aina nyingine. Baadhi ya bati zinaweza kuwa na gharama kubwa lakini ni imara sana.
  • Namna ya muonekano au muundo wa paa unaosababishwa na mtindo au muundo wa ramani ya nyumba yenyewe:
    Uchaguzi wa bati unaweza pia kusababishwa na namna nyumba yenyewe ilivyokaa kwa mfano bati yenye gable nyingi inafaa zaidi kwa bati nzuri wakati vigae vinavutia sana kwa bati yenye muonekano wa hip zaidi.
  • Ukarabati na matengenezo:
    Unaweza kuchagua bati kulingana na namna ulivyojiandaa wewe kufanya matengenezo kila baada ya muda gani. Kuna bati zitahitaji matengenezo miaka michache tu baada ya kununua au zinaweza kiharibika haraka kutokana na kuathiriwa na hali ya hewa wakati kuna bati au vigae ambavyo vinaweza kudumu kwa miaka mingi sana bila kuhitaji kuguswa kwa namna yoyote ile.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *