FANYA MAKADIRIO YA GHARAMA ZA UJENZI KITAALAMU SIO KWA MAFUNDI.
- Suala la gharama za ujenzi limekuwa ni suala lenye utata na linaloumiza sana vichwa vya watu sio tu watu wa kawaida na mafundi bali hata wataalamu wenyewe wa ujenzi. Hii ni kwa sababu makadirio ya gharama za ujenzi sio kitu kinaweza kufanyika kwa haraka kama wengi wanavyodhani wala sio kitu kinachoweza kupatikana kwa ukamilifu kamili badala yake kunaweza kuwa na upungufu au ongezeko. Sababu zinazopelekea hilo zinaweza kuwa mbalimbali na hutokea kwa miradi yote ya ujenzi kuanzia miradi ya watu binafsi mpaka miradi mikubwa ya serikali na miradi ya mashirika ya kimataifa.

- Lakini pamoja na changamoto hiyo bado unapaswa kuhakikisha kwamba unatafuta mtaalamu wa ukadiriaji majenzi badala ya kutumia mafundi ambao kwanza sio taaluma yao, pili sio eneo lao la uzoefu na tatu ni rahisi kukupotosha.

- Wataalamu wa makadirio ya gharama za ujenzi wenye uzoefu watakusaidia kwanza kuisoma michoro kwa usahihi na kuigawa kazi yote kwa hatua mbalimbali na kisha kukupa uwiano mzuri wa kazi katika utekelezaji na mgawanyo wa gharama mbalimbali za huduma ya ufundi kadiri ya vipaumbele.

- Wataalamu wa ukadiriaji majenzi kitaalamu wanaitwa Quantity Surveyors maarufu zaidi kama QS, hawa ni watu ambao wanajua kuitumia michoro na kuitafsiri kwa namna ya vifaa vya ujenzi katika kila hatua na kwa usahihi mkubwa. Hayo wanafanya kwa kutengeneza kwanza vifaa vya ujenzi kitaalamu tunaita Quantities kisha kuingiza bei ndani yake na kuja na uwiano wa gharama zote kwa ujumla mpaka usafirishaji na gharama zinazosindikiza gharama kuu.
- Ni rahisi na sahihi sana kutumia njia hii kupata makadirio ya gharama hizo.
- Karibu sana tukufanyie makadirio ya gharama za ujenzi wa mradi wako wowote wa ujenzi.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790.



Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!