NAMNA SAHIHI YA KUDHIBITI WIZI KWENYE MIRADI BINAFSI YA UJENZI UNAYONUNUA VIFAA.
Mara nyingi tumekuwa tukishauri kwamba mtu yeyote anayeamua kujenga kama mtu binafsi na wakati mwingine mpaka taasisi binafsi basi ni vyema suala la kununua vifaa vya ujenzi anunue mwenyewe japo kwa msaada wa ushauri na maelezo kutoka kwa mtu au kampuni inayomfanyia ujenzi.

Lengo la kushauri hivi ni kwa sababu mara nyingi mradi wa ujenzi ambao upande wa mteja unaamuliwa na mtu mmoja ni rahisi sana kutokea mivutano na kutokuelewana juu ya vifaa vya ujenzi kunakoweza kuathiri maendeleo ya mradi au hata kuvunjika kwa mahusiano na mradi wenyewe.
Hili mara nyingi husababishwa na mtu mwenye ushawishi kwa mteja kumpelekea habari kwamba mtu aliyemchagua kujenga sio mwaminifu kwenye kununua vifaa vya ujenzi na bila mteja kujua kama ni kweli au sio kweli tayari mivutano na malumbano hutokea na kupelekea kuharibika kwa mradi.

Hata hivyo mtu huyu anayepeleka habari anaweza kuwa anafanya uchonganishi tu kwa sababu mbalimbali kama vile kumuondoa aliyepewa kazi ili yeye anaufaike au labda ana kisasi na alieyepewa kazi au ana mtu wake ambaye anatamani ndiye apewe hiyo kazi au wakati mwingine pia yuko sahihi kwamba huenda aliyepewa kazi sio mwaminifu.
Hivyo ili kupunguza sehemu ya matatizo hay ani vyema na muhimu sana mteja mwenyewe akafanya manunuzi ili ajionee mwenyewe gharama hizo za ujenzi zilivyo kiuhalisia. Lakini pia ni muhimu kwa mteja kununua mwenyewe inasaidia kukwepa uchakachuaji au kununuliwa kwa vifaa visivyo na ubora kwa sababu tu ya tamaa ya aliyepewa kazi ya kununua vifaa kufanya uchakachuaji na kuchukua fedha zinazobaki.

Changamoto sasa ambayo huwa inakuja mara zote ni kwamba mara nyingi mteja hukosa muda wa kufuatilia na kununua vifaa hivyo humchagua mtu wa kumsaidia kwenye hilo la vifaa na kinachotokea ni kwamba huyo anayemchagua ndio huishia kumwibia mteja husika. Watu wengi huwaamini watu kwa sababu ni watu wao wa karibu au wameaminishwa kwamba ni watu watulivu na waaminifu na matokeo yako hao walioaminiwa ndio huishia kuwaibia.

Hili tumekutana nalo mara nyingi pale ambapo ndugu, jamaa na marafiki huishia kuwaibia wale waliowaamini. Imeshatokea kwetu kesi za mke kumuibia mume wake, mtoto kumuibia mzazi, mpwa kumuibia mjomba, mjukuu kumuibia babu mpaka mzazi kumuibia mtoto wake mwenyewe. Kutokana na ukaribu wa kimahusiano basi mhusika hushindwa kumchukulia hatua na wakati mwingine huishia kumuondoa tu au kumuacha na kumpangia majukumu mengine.
Sasa ili kuepuka hili ni muhimu sana kwamba maazimio yote na changamoto zote zinazoweza kujitokeza yafanyike mwanzoni mwa mradi na kila mtu awe mlinzi wa mwenzake huku mkandarasi aliyepewa kazi akisainishwa mkataba wa adhabu kali ikiwa atanyamazia wizi wa aina yeyote uliotokea.

Kuwekwe pia utaratibu wa makubaliano rasmi ya kuweka kikao cha kumpata yule ambaye atakuwa ameshiriki wizi mara moja baada ya kutajwa na kila mtu atawajibika kwa sehemu na kujieleza vya kutosha atakapobainika kujihusisha na vitendo hivyo.
Karibu tukufanyie kazi yako ya ujenzi kwa uaminifu mkubwa na kutengeneza mfumo wa uwajibikaji utakaohakikisha hakuna nafasi ya wizi au upotevu wa kifaa chochote huku uwajibikaji ukiwa ni wa kiwango cha juu kabisa.
Karibu sana
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.



Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!