UMUHIMU WA KUMILIKI NYUMBA YAKO MWENYEWE YA KUISHI

Ndugu Mdau wa Ujenzi

Nyumba Bora Ya Kuishi Ni Moja Kati Ya Ndoto Ya Kila Mtu Katika Maisha. Leo Tunaangazia Umuhimu na Faida za Kumiliki Nyumba Yako Mwenyewe Ya Kuishi Kwa Wale Ambao Bado Hawajaweza Kufikia Hatua Hii Lakini Hata Wale Waliofikia ni Muhimu Kujikumbusha.

-Kwanza kabisa kumiliki nyumba yako kunakupa uhuru mkubwa wa kuamua nini ufanye na nini usifanye katika mazingira yako, hakuna tena mtu yeyote wa kukupangia kwenye mazingira yako mwenyewe.

-Kumiliki nyumba yako kunakupa utulivu mkubwa ambao unaokosa kwenye nyumba ya kupanga, kwamba mwisho wa mwezi umefika na mwenye nyumba anataka kodi yake ni jambo linaloumiza sana kisaikolojia na wakati mwingine hata kudhalilisha utu.

-Kumiliki nyumba yako kunakuongezea heshima kubwa kijamii na hata katika familia yako, kitu ambacho kila mtu anahitaji ili kuhisi amekamilika, heshima hii japo sio hitaji la msingi lakini ni hitaji muhimu sana kisaikolojia

-Kumiliki nyumba yako kunakupa nafasi ya kuamua mipangilio yake, idadi ya vyumba na kila hitaji ambalo linaendana na hobi na utamaduni wako binafsi, kitu ambacho ni ngumu kukifanikisha kwenye nyumba za kupanga. Kumiliki nyumba ni kuishi aina ya maisha uliyoiota kwa miaka mingi. Ni kutimiza moja ya ndoto zako katika maisha.

-Kumiliki nyumba yako ni kupata ushindi mkubwa kijamii. Jamii zetu zinaamini kama bado hujamiliki nyumba yako bado maisha yako hayajakamilika, na kwa sababu sisi binadamu ni viumbe wa kijamii hili ni hitaji muhimu sana kulitimiza ili kuhisi umekamilika. Watu wote mpaka ndugu, jamaa na marafiki watakuweka kwenye nafasi ya tofauti kabisa na wanayokuweka sasa baada ya kumiliki nyumba yako na utaweza kuliona hilo wazi.

-Utaanza kuonekana mjanja na mtu unayejua ni wapi unaelekea na maisha yako kwa kumiliki nyumba yako na kwa sababu ukishakuwa mkubwa kidogo swali ambalo watu huuliza ni, umeshajenga?, hivyo utakuwa unakabiliana na swali hili kwa kujiamini kitu kitakachofanya watu waongeze imani kwako.

-Kumiliki nyumba yako ni mafanikio makubwa sana kifamilia, kuanzia watoto mpaka mwenza wako wataongeza imani na heshima kwako na hata wao watajihisi wamekamilika zaidi kisaikolojia.

-Kumiliki nyumba yako kunakupa fursa kulea watoto katika malezi sahihi na ambayo unayahitaji. Kama tunavyojua malezi ya siku hizi yamekuwa ni changamoto sana kutokana na utandawazi na ukisasa ambao kwa sehemu kubwa unaleta uharibifu mkubwa hasa kwa watoto ambao bado hawajajua lipi la kufanya na lipi la kuacha. Utaweza kuwa na udhibiti sahihi wa malezi kwa watoto na kuepuka kusaidiwa malezi na watu waliokosa maadili kijamii.

-Kumiliki nyumba yako kunakupa fursa ya kuanzisha shughuli ya kiuchumi nyumbani kwako ambayo itakuwa rahisi kuiendesha kwa sababu uko nayo karibu na inaweza kukuongezea kipato au kukupunguza gharama za maisha kama vile ufugaji au mradi mdogo wa mboga mboga.

-Kumiliki nyumba yako kutakupa fursa ya kuishi kwenye mazingira unayoyataka kwani utakuwa huru kuboresha mazingira yako kadiri unavyotaka mwenyewe na kuyafanya mazingira yako ya nje kuwa bora sana. Unakuwa huru kupanda hata mimea inayoendana na utamaduni wenu.

N:B Kumiliki Nyumba Yako Ya Kuishi ni Kumiliki Uhuru Zaidi wa Maisha Yako. Karibu Tukuisaidie Kumiliki Nyumba Yako Itakayokidhi Vigezo Vyote na Kukupa Furaha Unayoihitaji Baada Ya Kufanikisha Jambo Hili.

Na Architect Sebastian Moshi

Mawasiliano +255717452790.

1 reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *