GHARAMA ZA UJENZI

Gharama za ujenzi, – Gharama za ujenzi hutofautiana kutokana na aina ya jengo kwa maana ya matumizi, gharama ya kujenga godown, hospitali, hotel, shule, kanisa, msikiti, majengo ya biashara, majengo ya ofisi, makazi ya watu wengi, nyumba ya kuishi na aina nyingine za majengo bei zake ni tofauti na zimeainishwa na bodi lakini nao pia hawajachanganua kwa undani pia lakini pamoja na yote wastani wa bei ya kawaida kwa mazingira yetu ni Tshs 700,000 mpaka 750,000 kwa mita moja ya mraba (per square meter).

Hivyo utachukua mita za mraba za eneo unalojengo (built up area) utazidisha kwa hiyo 750,000 utapata gharama ya jengo. Kwa mfano unajenga ghorofa tano ambapo floor zote zina ufanano na eneo la floor ile ya chini(ground floor area) ni labda mita za mraba 250 utachukua 250 uzidishe mara 5 utapata ni mita za mraba 1,250 kisha utazidisha mara 750,000 utapata ni milioni 937,500,000 ndio bei yote ya ujenzi kwa  kila kitu kinachohusiana na huo mradi. Lakini huu ni wastani wa bei, inaweza kuongezeka au kupungua kutegemea sasa na mambo mengi sana. 

Kuanzia aina ya mradi matumizi na mambo mengine ambayo yanahitajika katika jengo husika, utakuta hotel labda unahitaji kuweka air conditions labda na mifumo ya computer ndani na vinginevyo ambapo nyumba ya kuishi ya kawaida unaweza usiweke hiyo inaenda mpaka kwenye mahoteli, hospitali, taasisi mbalimbali na maeneo mengine, hivyo hiyo bei inaweza kuongezeka au kupungua, huo ni wastani wa bei ya makadirio ya chini katika viwango vilivyopangwa na bodi hizi za ujenzi, inaweza kuongezeka au kupungua. Makadirio ya hizi bodi kulingana na mradi yanapanda mpaka milioni 1.2 kwa mita moja ya mraba na kushuka mpaka 600,000 kutegemea na matumizi au aina ya jengo. Wakati mwingine mtaani mambo hufanyika kiholela hivyo usishangae kusikia mtu amejenga aidha kwa gharama kubwa au ndogo sana lakini ubora na uhitaji ukawa haujafikiwa, wewe usiyejua undani wa mradi husika ni vigumu kufahamu utaona tu kwa nje na kutoa maoni yako kwa kadiri unavyoona au kufikiri.

Architect Sebastian Moshi

Mawasiliano +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *