SAKAFU YA TERRAZO

Sakafu ya terrazzo ni aina ya sakafu inayotengenezwa kwa mchanganyiko wa malighafi mbalimbali zinazotengeneza aina nyingine za sakafu. Inajumuisha vipande vidogo vidogo vya marble, udongo, granite, quartzite, kioo na malighafi nyingine zinazoendana na matokeo tarajiwa kisha kuchanganywa na kemikali nyingine kama saruji ambayo ndio inazikamatia pamoja.

SAKAFU YA TERRAZO

Vipande vya chuma huweza kutumika kuchanganywa ili kutengeneza mtiririko unaovutia au kubadili rangi au mpangilio wa muonekano wa uso wa sakafu yenyewe. Mwisho humaliziwa kwa kupakwa rangi ya polish ili kubaki na ile finishing nzuri na laini ya uso wa sakafu au ukuta wa terrazzo.

FAIDA YA SAKAFU YA AINA TERRAZO

-Terrazo inadumu miaka mingi sana bila kuharibika wala kukwaruzika kwa sababu inajumuisha malighafi nyingi ambazo ni imara kwenye mchanganyiko wake na hauruhusu maji kupenya hivyo kuleta uimara.

-Terrazo zinafaa sana kwa matumizi kwenye maeneo yenye watu wengi na maeneo ya umma bila kuathirika kutokana na uimara wake unaosababishwa na mchanganyiko imara sana.

-Hata pale terrazo inapokuwa imepoteza ubora wake baada ya miaka mingi sana inaweza kurekebisha kiurahisi na kupakwa rangi ya polish na kuonekana mpya tena.

-Gharama ndogo inayohitajika kuifanyia ukarabati terrazzo na umri mrefu sana ambao inaodumu maana yake ni sawa na inauzwa kwa gharama nafuu sana.

-Kwa kuwa terrazzo inatenengenezwa kutokana na aina nyingi za urembo na malighafi ina uwezo wa kufanya katika staili nyingi za kupendeza. Hii inawarahishia wasanifu majengo kuwa huru katika ubunifu.

-Terrazo ni rafiki wa mazingira. Terrazo inaweza kutengenezwa kwa malighafi ambazo zinaweza kurudia kutumika ten ana ten ana yanayoweza kupatikana katika mazingira yoyote na kubadili mwonekano uliozoeleka.

-Terrazo inaweza kutumika katika mazingira ya ndani na mazingira yan je ya jengo. Terrazo zinawekwa kila mahali kwenye korido, kwenye kumbi, majengo ya kanisa na mikusanyiko mingine, kwenye baraza, veranda, kwenye ngazi n.k. Pia unaweza kuweka terrazzo katika kaunta za jikoni, bafuni, kwenye swimming n.k,

SAKAFU YA TERRAZO

CHANGAMOTO ZA SAKAFU AINA YA TERRAZO.

-Gharama za mwanzoni za terrazzo ni kubwa sana ukilinganisha na sakafu za aina nyingine. Unafaa wa gharama kwenye terrazzo unakuja kwa muda mrefu kwani baada ya miaka mingi gharama za terrazzo zinakuja kwa ndogo lakini gharama za mwanzoni ni kubwa.

-Terrazo huwa za baridi sana nyakati za baridi na hivyo kuleta usumbufu kwa watu wanaozikanyaga wakiwa peku katika mazingira ya baridi kali.

-Zina ugumu na changamoto zaidi kwenye kuzijenga ukilinganisha na sakafu za aina nyingine.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *