SAKAFU YA MBAO

Sakafu ya Mbao ni sakafu yoyote iliyotengenezwa kwa kutumia malighafi za mbao. Sakafu ya mbao ni kati ya machaguo ya sakafu ambayo hutumika sana kwa maeneo mbalimbali na hupatikana na ubunifu, rangi na aina tofauti tofauti. Miti ya miwale au bamboo hutumika sana pia kama aina ya sakafu yam bao.

SAKAFU YA MBAO

FAIDA ZA SAKAFU ZA MBAO

-Ni uwekezaji wa muda mrefu, japo zina gharama kubwa mwanzoni lakini hutahitaji kuzibadilisha.

-Sakafu za mbao zinaweza kupatikana kwa aina nyingi sana hivyo unaweza kuwa na machaguo mengi sana ya aina tofauti tofuati. Kuna kila namna ya muonekano na mpangilio na zote ni tofauti, kwa hiyo inatoa fursa ya kupata namna utakayoipenda wewe. Unaweza pia kuchanganya aina hizi ukapata na ukapata muonekano bora zaidi.

-Mbao zina ubora usioisha. Tofauti na aina nyingine za sakafu mbao ni aina ambayo thamani yake haishuka na kadiri miaka inavyosogea mbele ndivyo ubora wake unaongezeka zaidi.

-Mbao ni rahisi kusafisha na hazishiki sana uchafu, zina uwezo mkubwa wa kukwepa vumbi kwa sababu hazina kabisa umemesumaku wa kuvuta vumbi.

-Sakafu za mbao hazivutii sana wadudu kama vile parasite.

-Ni rahisi kuziweka au kuzijenga katika sakafu husika.

SAKAFU YA MBAO

CHANGAMOTO ZA SAKAFU ZA MBAO.

-Gharama zake ni kubwa kwa ujumla

-Zinaweza kushambuliwa na mchwa.

-Haizihitaji kabisa kuingiwa na maji.

-Ni rahisi kupata mikwaruzo hivyo zinahitaji umakini wa hali juu.

-Hazifai kutumika kila mahali, kwa mfano sehemu zenye majimaji kama vile bafuni na jikoni.

Architect Sebastian Moshi

255717452790

Tembelea website yetu www.ujenzimakini.com, kusoma makala bora sana za ujenzi

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *