AINA KUU MBILI ZA KUTA KUTOKANA NA UIMARA

Baada ya kuangalia aina kuu mbili za kuta kutokana na matumizi sasa tuangalie aina kuu mbili za kuta kutokana na uimara na kile inachojumuisha.

Ukuta Mzito na Mpana wa Matofali

AINA KUU MBILI ZA KUTA KUTOKANA NA UIMARA NA KILE INACHOJUMUISHA

  1. Kuta nzito pana
  2. Kuta nyepesi nyembamba
  1. Kuta Nzito Pana – Hizi ni kuta ambazo hutengenezwa kwa matofali ya kuchoma au matofali ya saruji. Miaka ya zamani sana kabla teknolojia ya matofali haijaenea kuta hizi kwa sehemu kubwa duniani zilijengwa kwa mawe. Kuta hizi mara nyingi hujengwa juu ya boriti/beam ambayo ndio hubeba uzito wa ukuta husika kwa maana kuta hizi huwa ni nzito sana.
Ukuta Mzito na Mpana wa Mawe

Mara nyingi kuta hizi huunganishwa kwa kushikiliwa na gundi ya plasta ya saruji iliyoleweshwa na kisha hupakwa plasta pande zote mbili za kuta ili kuleta muonekano unaovutia zaidi.

2. Kuta Nyepesi Nyembamba – Hizi ni kuta ambazo ni nyepesi na kwa kawaida hujengwa kwa haraka sana. Kuta hizi huwa hazihitaji kukaa juu ya boriti/beam inayobeba uzito wake kwani huwa ni nyepesi na inaweza kuwekwa popote juu ya sakafu/slab husika.

Kuta Nyepesi na Nyembamba za Mbao Nyepesi na Vioo

Mara nyingi kuta nyepesi hutengenezwa kwa kuanza kwanza kutengeneza fremu yak uta husika na kisha kutengeneza kuta yenyewe ambayo huingia ndani ya fremu hiyo. Mara nyingi kuta nyepesi hutengenezwa kwa malighafi kama mbao nyepesi, chuma nyepesi, kioo, bodi za paneli zinazotengenezwa kwa malighafi mbalimbali n.k.,

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *