AINA ZA MADIRISHA

Kuna namna mbili za kuyaeleza madirisha

  1. AINA ZA MADIRISHA KUTOKANA NA MUUNDO
  2. AINA ZA MADIRISHA KUTOKANA NA MALIGHAFI ILIYOTUMIKA KUYATENGENEZA

AINA ZA MADIRISHA KUTOKANA NA MUUNDO.

-MADIRISHA YASIYOSOGEA/FIXED WINDOWS – Haya ni madirisha rahisi zaidi katika aina zote za madirisha, ni madirisha yasiyofungwa wala kufunguliwa hivyo yanatumika zaidi maeneo yenye hali ya hewa ya baridi kali

DIRISHA LISILOSOGEA/FIXED WINDOW

-MADIRISHA YA BAWABA/CASEMENT WINDOWS – Hii ni aina ya madirisha ambayo mara nyingi hufungukia upande wa nje ya nyumba badala ya ndani hivyo kuwa rahisi kutumika. Japo hata hivyo kutokana na kufungukia ndani kuna maeneo huwa hayawezi kutumika kwa mfano eneo ambalo kwa nje nyumba ina uchochoro mwembamba sana au korido ambayo inatumika sana. Madirisha haya mara nyingi hutengenezwa kukabiliana na upepo mkali na mvua inayopiga kwenda ndani hivyo ndio maana hubaki kufungukia upande wan je wa nyumba.

DIRISHA LA BAWABA/CASEMENT WINDOW

-MADIRISHA YANAYOTEMBEA/SLIDING WINDOWS – Hii ni aina ya madirisha ambayo hutembea katika reli yake yenyewe. Changamoto ya madirisha haya ni kwamba dirisha haliwezi kufunguka lote, linaweza kufunguka nusu au robo lakini lazima kuna kipande kitabaki kimefunga. Faida ya madirisha haya ni kwamba hayahitaji nafasi ya nje au ya ndani ya chumba kufungukia bali yanatembea katika eneo lake la dirisha pekee, hivyo yanafaa sana kutumika katika eneo ambalo kwa nje hakuna nafasi ya dirisha kufungukia.

DIRISHA LINALOTEMBEA/SLIDING WINDOW

Itaendelea.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *