MADIRISHA YA MBAO

Madirisha ya mbao ni aina ya madirisha ambayo yanatengenezwa kwa kutumia mbao zilizovunwa kutoka kweye aina mbalimbali za miti. Kwa miaka mbao imekuwa ikitumika katika kutengeneza madirisha japo kwa sasa utumiaji wa mbao katika madirisha umepungua sana.

DIRISHA LA MBAO

FAIDA ZA MADIRISHA YA MBAO

-Mwonekano, mwonekano unaovutia ni moja ya sababu watu wengi hupendelea madirisha ya mbao. Malighafi za asili kama mbao huwa na mwonekano wa kipekee sana ndio sababu hata aina nyingine za madirisha hupenda kuiga mwonekano wa mbao japo yanaweza kuwa sio madirisha yam bao. Malighafi ya mbao kwa kawaida hupokea vizuri rangi inapopigwa na kuw ana mwonekano bora zaidi ya kawaida.

-Haipitishi joto, mbao tofauti na chum ana aluminium haipitishi joto hivyo hutunza kiwango cha joto kilichopo ndani ya nyumba bila kuruhusu baridi kali au joto kuingia ndani. Hii hufanya yafae zaidi kwenye maeneo ya baridi kali.

-Madirisha yam bao yana uwezo mkubwa wa kuzuia kelele kuingia ndani ya nyumba zaidi kuliko madirisha ya aina nyingine.

-Kudumu muda mrefu, tafiti zinaonyesha kwamba madirisha ya mbao yanadumu muda mrefu sana kuliko aina nyingine za mdirisha, yanadumu zaidi ya umri wa kawaida wa mtu hivyo yanatoa nafasi ya kupunguza gharama katika kuyabadilisha.

-Hayatanuki kutokana na joto, madirisha ya mbao ndio madirisha ambayo yana nafasi ndogo sana ya kutanuka kutokana na joto hivyo unaweza kuchagua aina yoyote ya urembo na ikafaa bila kuwa na mabadiliko wakati wa joto kali.

DIRISHA LA MBAO

CHANGAMOTO ZA MADIRISHA YA MBAO.

-Madirisha ya mbao yanahitaji kupigwa rangi, na yanahitaji kupigwa mara kwa mara kwa sababu bila kutunzwa vizuri huwa rahisi kuharibika kutokana na unyevu au kupauka na kupoteza mvuto.

-Kushambuliwa na wadudu, madirisha yam bao yako kwenye hatari kubwa ya kushambuliwa na wadudu hasa wadudu wa aina ya mchwa au sisimizi, hivyo yanahitaji uangalifu na kuhudumiwa mara kwa mara.

-Gharama kubwa za mwanzoni, madirisha ya mbao ni aina ya madirisha ambayo hugharamu sana mwanzoni japo yana faida ya kudumu muda mrefu lakini yanahitaji maandalizi makubwa ya gharama za kuyaweka.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *