MADIRISHA YA CHUMA.

Madirisha ya chuma ni aina ya madirisha yanayotengenezwa na malighafi imara sana ya madini ya chuma ambapo yanakuwa na fremu nyembamba hivyo kuweza kuongeza uwazi mkubwa zaidi wa dirisha wa kuona upande wa nje. Chuma sio rahisi kuikata kama ilivyo kwa aluminium hivyo kazi kubwa inafanyika kiwandani zaidi kuliko katika eneo la ujenzi.

DIRISHA LA CHUMA

FAIDA ZA MADIRISHA YA CHUMA

-Kutokana na uimara wa chuma eneo la fremu huwa jembamba sana hivyo inakuwa rahisi kupata upana wa kutosha mtu kupata mwonekano wa nje kwa uwazi mkubwa.

-Madirisha ya chuma hayahitaji matengenezo ya mara kwa mara sana.

-Madririsha ya chuma sio rahisi kuvunjika wala kukunjika.

-Madirisha ya chuma huwa na sifa za kuongeza au kupunguza joto hivyo husaidia kupunguza gharama za kuongeza au kupunguza joto kwa njia za kisasa ambazo huhitaji nishati nyingi inayoongeza sana gharama za kuliendesha jengo.

-Madirisha ya chuma yana uwezo mkubwa wa kupambana na moto na kuuzuia kusambaa.

-Madirisha ya chuma yanatengenezeka kiurahisi bila kuhitaji gharama kubwa.

DIRISHA LA CHUMA

CHANGAMOTO ZA MADIRISHA YA CHUMA.

-Madirisha ya chuma ni mazito sana kubebeka.

-Madirisha ya chuma yanahusisha gharama kubwa sana.

-Chuma huathiriwa na maji ya chumvi chumvi ambayo hupelekea kupata kutu na hata kutoboka hovyo inapoteza sifa za kutumika baadhi ya maeneo hasa maeneo yenye maji yenye chumvi.

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *