PAA LA VIGAE VYA MAWE

Kuna aina fulani ya mawe yanayotokana na miamba ya aina ya mwamba moto ambayo hukaa muundo wa bapa hivyo baada ya kuchongwa kidogo na kuwa myembamba hutumika kama vigae kuezeka kwa kupangiliwa kwa umakini mkubwa.

UEZEKAJI WA PAA LA VIGAE VYA MAWE

FAIDA ZA PAA LA VIGAE VYA MAWE

-Paa la vigae vya mawe ni zuri sana kwa kutunza hali ya hewa ya ndani na kupunguza gharama za nishati katika kudhibiti hali ya hewa. Hivyo hali ya hewa ya joto au baridi haiathiri sana hali ya hewa ya ndani.

-Paa la vigae vya mawe linazuia moto kusambaa kwa uhakika mkubwa sana hivyo yanafaa sana kwenye nyumba zilizopo maeneo yenye msitu unaoshambuliwa na moto mara kwa mara.

-Paa la vigae vya mawe ni rafiki wa mazingira kwa sababu mawe haya ya vigae hayahitaji kupitia viwandani na katika michakato inayohusisha matumizi makubwa ya nishati hasa umeme mpaka kukamilika.

-Paa la vigae vya mawe linakaa miaka mingi sana bila kuhitaji kubadilishwa, linadumu miaka zaidi ya 100 bila kuhitaji mabadiliko yoyote.

-Paa la vigae vya mawe halihitaji ukarabati au matengenezo ya mara kwa mar ana linadumu sana

-Paa la vigae vya mawe linaweza kupatikana kwa rangi tofauti tofauti.

UEZEKAJI WA PAA LA VIGAE VYA MAWE

CHANGAMOTO ZA PAA LA VIGAE VYA MAWE

-Paa la vigae vya mawe ni zito sana, uzito wa paa la mawe unaweza kuwa hata zaidi ya mara tano ya uzito wa vigae vingine vya kawaida hivyo inahitaji nguvu nyingi zaidi na imara kubeba mzigo mzito wa paa kitu ambacho kitaongeza gharama kwenye mfumo wa mihimili ya jengo.

-Paa la vigae vya mawe ni la gharama kubwa sana ukilinganisha mwanzoni ukilinganisha na mapaa ya vigae vingine, lakini kwa kuwa inadumu muda mrefu inaweza kuwa ni gharama nafuu kwa baadaye kwa sababu hutahitaji kubadilisha badilisha paa kama malighafi nyingine.

-Paa la vigae vya mawe linahitaji utaalamu wa hali ya juu zaidi kuezeka kuliko mapaa mengine na hivyo utahitaji kupata mtaalamu ambaye ni wa gharama kubwa zaidi.

PAA LA VIGAE VYA MAWE VILIVYOCHAKAA

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *