PAA LA VIGAE VYA UDONGO.

Vigae vya udongo ni aina ya vigae ambavyo vimekuwa vikitumika kwa miaka mingi sana na malighafi ya udongo imekuwa inapatikana kiurahisi na rahisi pia kuitengeneza katika maumbo mbalimbali ambayo yanarahisha mtiririko rahisi wa maji kwenye paa. Vigae vya udongo hupendeza na kuvutia.

PAA LA VIGAE VYA UDONGO

FAIDA ZA PAA LA VIGAE VYA UDONGO

-Paa la vigae vya udongo linadumu sana hata zaidi ya miaka 100 bila kufanya ukarabati wala matengenezo yoyote zaidi ya kufanya usafi peke yake.

-Paa la vigae vya udongo ina uwezo wa kumudu hali ya hewa yenye changamoto nzito kama vile upepo mkali kwa sababu ya uimara na uzito.

-Paa la vigae vya udongo linaongeza thamani ya nyumba isiyopungua kiurahisi.

-Vigae vya udongo ni rafiki wa mazingira kwani zinatengenezwa kwa kutumia malighafi ya asili bila kuchanganya na kemikali nyingi za viwandani.

-Paa la vigae vya udongo linatunza hali ya hewa ya ndani ya nyumba hivyo wakati wa joto kali na wakati wa baridi kali hali ya hewa ya ndani ya nyumba haiathiriki sana hivyo husaidia pia kupunguza gharama za nishati ya umeme zinazotumika kuongeza au kupunguza joto ndani ya nyumba kama vile kiyoyozi, feni, n.k.,

-Paa la vigae vya udongo linapatikana katika aina na staili nyingi pamoja na rangi mbalimbali hivyo inasaidia kuvutia san ana kuendana na aina mbalimbali za ubunifu.

UEZEKAJI WA VIGAE VYA UDONGO

CHANGAMOTO ZA PAA LA VIGAE VYA UDONGO.

-Paa la vigae vya udongo lina gharama kubwa ukilinganisha na bati.

-Paa la vigae vya udongo ni zito sana ukilinganisha na paa la bati au Harvey tiles hivyo inaweza kuhitaji kuongeza uimara wa jengo kuweza kumudu mzigo wa vigae.

-Paa la vigae vya udongo vinahitaji kazi kubwa sana kuezeka hivyo inahitajika utaalamu mkubwa na gharama zaidi ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa usahihi.

-Vigae huweza kuvunjika zinapoangukiwa na kitu kizito sana kama vile mtu mkubwa au jiwe kubwa.

AINA TOFAUTI ZA VIGAE VYA UDONGO

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *