MIFUMO YA ZIMAMOTO KWENYE JENGO.
-Mifumo ya zimamoto ndio pengine huduma muhimu zaidi katika jengo kwani lengo lake kuu ni kulinda maisha ya watu wanaolitumia jengo na mali zilizopo ndani ya jengo husika.
MIFUMO YA ZIMAMOTO IMEGAWANYIKA KATIKA SEHEMU KUU TATU.
-Sehemu Ya Kwanza ni mapipa makubwa ya maji yaliyochimbiwa chini ya ardhi au yaliyopo juu ya jengo yanayojulikana kama mapipa ya maji ya kuzima moto.
-Sehemu Ya Pili ni mfumo wa pampu za kusukuma maji.
-Sehemu Ya Tatu ni mtandao mkubwa wa bomba zinazotoka kwenye mapipa kwenda maeneo yote ya jengo ambazo ziko katika aina kuu mbili, moja ni zile zenye mitungi na mabomba zinazoratibiwa na watalaamu wa kuzima moto(fire hydrants and hose reel) na nyingine ni zile zinazojiendesha zenyewe(fire sprinklers), kwa usalama zaidi inashauriwa kwamba ni muhimu jengo kuwa na aina zote mbili za mabomba.
AINA ZA MIFUMO YA ZIMAMOTO
-Aina ya kwanza ni mfumo wa mitungi iliyosimama wima na mabomba inayoratibiwa na wataalamu wa zimamoto(Fire hydrant)
-Aina ya pili ni mfumo unaofungwa moja kwa moja kwenye jengo na kujiendesha wenyewe (Fire sprinklers)
MFUMO WA MITUNGI NA MABOMBA
Huu ni mfumo unaohusisha mtungi uliosimama wima pembeni ya bomba au mabomba marefu yaliyokunjwa na kusokotwa kwenye rola. Ikiwa kuna ajali ya moto imetokea wataalamu wa zimamoto hukunjua mabomba haya kisha kuchomeka kwenye mtungi(hydrant) na mtungi husukuma maji kwa presha kubwa ambayo hutoka na kuelekezwa sehemu maalumu inayowaka moto, huwa inahitaji mtaalamu mbobezi wa zimamoto kufanya kazi hii.
MFUMO WA UNAOFUNGWA MOJA KWA MOJA KWENYE JENGO(FIRE SPRINKLERS)
Huu ni mfumo ambao hufungwa juu kwenye “ceiling board”, ambapo mtandao wa mabomba huwekwa kisha kila baada ya umbali fulani kunakuwepo na koki ambayo inakuwa na kitu kama balbu yenye kimiminika ndani ambapo balbu hii inazuia maji yasitoke nje. Inapotokea moto na kimiminika kile kupata joto na hutanuka kisha kupasua balbu hivyo moja kwa moja maji hutoka kwenye koki kwa pressure kubwa. Tofauti kati ya mifumo hii miwili ni kwamba mfumo wa (fire sprinkler) hujiendesha wenyewe moja kwa moja pale moto unapotokea lakini mfumo wa mitungi na mabomba(fire hydrant) unahitaji wataalamu wa zimamoto kuuendesha baada ya wahusika kutoa taarifa kwamba kuna ajali ya moto imetokea eneo husika.
-Watafiti wa ajali za moto wanasema kwamba mfumo wa (fire sprinkler) ni mzuri zaidi na hulinda mali na maisha ya watu kwa zaidi ya asilimia 80% zaidi.
Hata hivyo kitaalamu inashauriwa kuwa na mifumo yote miwili kwa pamoja.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!