SHERIA ZA BODI YA UJENZI(CRB) ZINAZOSIMAMIWA NA (OSHA) JUU YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA UJENZI NA ADHABU ZAKE.

Hizi ni sheria zinazotungwa na kutekelezwa na bodi ya ujenzi na ukandarasi “Contractors Registration Borad(CRB)” na kusimamiwa na wakala wa serikali wa usalama na afya mapali pa kazi (OSHA) kama ifuatavyo.

USALAMA MAHALI PA UJENZI

-Kila mkandarasi ana wajibu wa kumpatia kila mtu aliyeko katika saiti ya ujenzi vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya kujilinda anapokuwa katika mahali pa ujenzi kama vile kofia ngumu(helmet), viatu vigumu, overall au kikoi(reflector), gloves, miwani n.k, kulingana na aina ya kazi anayofanya mhusika na kuhakikisha kwamba muda wote vifaa vyote vinatakiwa vimevaliwa na mhusika.

-Mkandarasi anapaswa kuhakikisha kwamba kila ajali inayotokea kwenye eneo la ujenzi inajazwa kwenye kitabu cha kuripoti ajali za saiti husika, iwe ndogo au kubwa kwa kuanzia na jina la mhanga, kazi yake, aina ya ajali, eneo ilipotokea, muda na tarehe, maelezo ya kimazingira ilivyotokea na hatua zilizochukuliwa baada ya kutokea ajali hiyo.

MFANYAKAZI ANAPASWA KUVAA VIFAA VYA KUJIKINGA NA AJALI MAHALI PA UJENZI MUDA WOTE

-Kushindwa kutekeleza hiyo sheria hapo juu utakabiliwa na adhabu ya kupigwa faini ya asilimia 0.1% ya gharama yote ya mradi huo au Tshs 100,000 ikiwa faini hiyo ya 0.1% ya gharama za mradi wa ujenzi husika haifiki Tshs 100,000.

-Eneo lote ambalo mradi wa ujenzi unafanyika(construction site) linatakiwa kuzungushiwa uzio(hoarding) na kosa la kushindwa kufanya hivyo litapelekea kukabiliwa na adhabu ya kutozwa faini inayolingana na asilimia 0.5% ya gharama zote za mradi wa ujenzi husika au Tshs 200,000 ikiwa asilimia 0.5% ya gharama zote za ujenzi husika hazifiki Tshs 200,000.

ENEO LOTE AMBALO UJENZI UNAFANYIKA(CONSTRUCTION SITE) LINATAKIWA KUZUNGISHIWA UZIO(HOARDING)

-Kila mkandarasi anapaswa kuhakikisha kwamba kila mfanyakazi aliyepo katika eneo la ujenzi anapatiwa vifaa vyote na mavazi yote ya kujilinda na kosa la kutofanya hivyo litapelekea adhabu ya kutozwa faini ya Tshs 20,000 kwa kila mtu mmoja ambaye hana vifaa na mavazi hayo ya kujilinda katika eneo la ujenzi.

FAINI YA TSHS 20,000 ITATOZWA KWA KILA MTU ATAKAYEKUTWA HANA VIFAA VYA KUJIKINGA NA AJALI ZA ENEO LA UJENZI(PPE)

-Kila mkandarasi ana jukumu la kuhakikisha kwamba kwenye eneo la ujenzi kuna vifaa vyote vya kukabiliana na ajali ya moto pamoja na kuwepo kwa eneo la kujisaidia na kuoga sambamba na beseni(sink) la kunawia mikono, ambapo kushindwa kutekeleza hilo kutapelekea adhabu ya kutozwa faini ya Tshs 50,000.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *