LENGO LAKO LIWE NI UBORA

Pale unapoamua kufanya kitu chochote kinachokugharimu fedha hasa fedha nyingi mara nyingi unafanya hivyo kwa sababu kitu kile kina manufaa makubwa kwako na kinaenda kuongeza thamnai kubwa kwako na kwenye maisha yako. Kwa hiyo sasa kitu ambacho kinakwenda kuboresha maisha yako na kuongeza thamani kwako na kwa maisha yako na kinachokugharimu fedha nyingi kinastahili kupewa uzito mkubwa ili kukupa thamani kubwa na ambayo hutaijutia.

FANYA LENGO KUU KWENYE MRADI KUWA NI UBORA

Sasa, hali kadhalika unapofikia maamuzi ya kujenga nyumba na ukaanza kuchukua hatua basi jambo la kwanza unalopaswa kuweka kichwani ni kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa ubora wa hali juu. Inaweza kusababisha ongezeko kidogo la gharama kwako lakini itakulipa sana mbeleni na kukuepusha na majuto na kuonekana ni mtu mjanja na mwenye akili, jambo litakalokuongezea hadhi kwako binafsi na hata na watu waliokuzunguka.

UBORA WA KAZI YAKO UTAKUONGEZEA HESHIMA NA HADHI KWENYE JAMII

Unapofikiria kujenga usikimbilia kufikiria bei peke yake au bei kwanza kabla hujafikiria ni namna gani utafanya kazi nzuri, yenye viwango vya hali ya juu na itakayokuwa mfano bora kwa kila mtu bila kujali ukubwa wake. Jambo hilo litakupa furaha binafsi ya muda mrefu na kukufanya uonekane uko makini hata kwa wale waliokuzunguka, lakini pia utayafurahia matunda ya maamuzi yako sahihi kwa muda mrefu sana.

UTAFURAHIA MATUNDA YA MAAMUZI YAKO SAHIHI KWA MIAKA MINGI

Kwa hiyo kuanzia kwenye kutengeneza ramani ya jengo lenyewe mpaka kwenye kuchagua watu sahihi wa kusimamia ujenzi huo, kwenye kuchagua malighafi sahihi zinazoendana na mradi husika pamoja na gharama zake.

KWENYE KILA HATUA KIPAUMBELE KIWE NI UBORA, KUANZIA MTU WA KUCHORA RAMANI MPAKA KUWEKA SAMANI ZA NDANI.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *