KUTANA NA MTAALAMU MSHAURI WA UJENZI KABLA HUJAANZA CHOCHOTE

Makosa mengi yanayotokea kwenye kazi za ujenzi mara nyingi huwa yaanzia mwanzoni kabisa mwa mradi au mteja kuwa na mtazamo usio sahihi kuhusu ujenzi na hivyo safari yake nzima ya mradi wa ujenzi kuathiriwa na mtazamo usio sahihi juu ya huo mradi wake ukilinganisha na uhalisia wa mambo yenyewe yalivyo au ambavyo huwa.

Hivyo utakuwa umefanya jambo muhimu na la maana sana endapo utakutana na mtaalamu wa masuala ya ujenzi kabla ya kuanza chochote juu ya mradi wako wa ujenzi ambapo mtajadili kwa marefu na mapana juu ya kila kitu kinachoenda kufanyika pamoja na changamoto zake kuanzia mwanzo kwenye kuchora ramani, upatikanaji wa vibali vya ujenzi mpaka kujenga na kukamilisha mradi wote wa ujenzi na kuanza kutumika kwa jengo.

KUWA MTAZAMO SAHIHI NA TAARIFA SAHIHI KABLA YA KUANZA MRADI WA UJENZI

Hata kama ulikuwa na uzoefu kutokana na miradi ya nyuma bado huwa kuna mabadiliko mengi nay a kasi sana yanayoendelea hasa kwenye mamlaka zinazosimamia ujenzi, lakini pia mara nyingi kwa mtu hauko kwenye fani ya ujenzi kuna mambo mengi huwa unasahau.

Kwa kukutana na mtaalamu wa ujenzi mkajadili kwa marefu na mapana itasaidia kukujengea mtazamo sahihi ambao utakaokuongoza katika mradi wako unakwenda kufanyika.

Karibu sana kwa ushauri wa kitaalamu wa kabla ya mradi kuanza

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

4 replies
  1. francis
    francis says:

    Kwa hakika ,kila kitu ni mipango na maandalizi..na katika ujenzi ni vivyo hivyo. Na hii inasaidia sana kuepukana na matokeo hasi kwa baadae,katika kazi na katika makubaliano. Asante sana

    Reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *