KUDHIBITI UBORA WEKA MSIMAMIZI WA NJE KWENYE MRADI WAKO WA UJENZI.

Kwenye miradi mikubwa ya ujenzi ambayo hufuata taratibu zote zilizowekwa mambo mengi huwekwa kwenye maandishi ikijumuisha viwango ambavyo vinategemewa kufikiwa, hata mikataba ya miradi hii huingiwa kwa masharti ambayo yanalazimisha kila kitu kilichopangwa kufikiwa katika viwango vilipangwa na kwa mategemeo ya mteja.

KWENYE MIRADI MIKUBWA YA UJENZI ILIYOFUATA UTARATIBU SAHIHI UNAOFUATWA HUDHIBITI UBORA

Lakini inapokuja kwenye miradi midogo au miradi mikubwa lakini haijafuata taratibu sahihi zilizopangwa na mamlaka husika huwa hakuna namna ya kudhibiti ubora. Kwanza mteja mwenyewe mara nyingi sio rahisi kujua viwango sahihi vya ubora lakini pia mradi hutolewa labda ni kwa mkandarasi peke yake bila kuwepo washauri wa kitaalamu wa kumsimamia mkandarasi kuhakikisha anafikia viwango vilivyopangwa au basi angalau hafanyi makosa ya kiufundi yatakayoleta madhara baadaye au yatakayoshindwa kuleta matokeo yanayotarajiwa kwa mradi husika.

KWENYE MIRADI AMBAYO HAIJAFUATA TARATIBU ZOTE ZA UJENZI UNAPASWA KUWEKA MTAALAMU KWA AJILI YA KUDHIBITI UBORA BADALA YA KUMWACHIA MKANDARASI PEKE YAKE KUFANYA ATAKAVYO

Hivyo katika kudhibiti ubora na kuhakikisha matokeo yanayotegemewa yanafikiwa bila kuletewa sababu za utetezi zisizo na manaufaa yoyote kwa mteja ni muhimu sana kuwepo mtaalamu anayesimamia ubora na viwango sahihi vinavyotarajiwa kufikiwa. Kwanza kabisa kuwepo kwa mtu wa nje anayesimamia ubora kutamfanya mkandarasi kufanya kazi yake kwa makini zaidi na kuepusha uzembe, tamaa na usimamizi hafifu. Lakini pia kuwepo kwa msimamizi anayedhibiti ubora wa mradi kutasaidia kuongeza thamani ya mradi kwani kwa mtaalamu huyu kuja na mapendekezo kadhaa ya kuboresha zaidi mradi ambayo baadhi yanaweza kuingizwa kwenye utekelezaji na kuleta matokeo bora zaidi. Mtaalamu wa kudhibiti ubora anapaswa kuwa mshauri wa kitaalamu mwenye uwezo na uzoefu katika kusimamia miradi hii kwa viwango vya juu.

MTAALAMU WA KUDHIBIRI UBORA ATASAIDIA KUEPUSHA UZEMBE, TAMAA NA USIMAMIZI HAFIFU.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *