CHANGAMOTO ZA MATUMIZI YA KIWANJA
Watu wengi wamekuwa wakikutana na changamoto za kusumbuliwa na mamlaka hasa halmashauri za miji, manispaa na majiji pale wanapokuwa wanafuatilia vibali vya ujenzi kutokana na suala zima la kigezo cha matumizi ya kiwanja.
Mara nyingi hasa miaka ya hivi karibuni kupata kibali cha ujenzi wa eneo lako suala la matumizi ya kiwanja limekuwa ni changamoto kubwa sana kwa baadhi ya watu kwa sababu kuna matumizi ya kiwanja yanayokaribiana sana kiasi kwamba mtu unaweza kufikiri uko sahihi na bado ukajikuta unazuiliwa. Kumekuwa kuna utofauti mdogo sana kati ya matumizi ya kiwanja kwa makazi biashara na makazi ya kawaida na hivyo unaweza kupeleka michoro ambayo ni makazi ya kawaida na bado ikaonekana kwamba ni makazi baishara, kitu ambacho kitakupa wakati mgumu.
Hivyo ni muhimu zaidi kuwa makini tangu mwanzoni au kufanya kazi na mtu anayeelewa vizuri usumbufu uliopo kwenye suala la matumizi ya kiwanja na hata vigezo vingine vya kiwanja kuendana na aina ya jengo/majengo unayotaka kujenga katika kiwanja husika vinavyoweza kukupunguzia usumbufu wakati unafanya ufuatiliaji wa kibali cha ujenzi.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!