FANYA KAZI NA WATU WANAOAMINIKA, KUWA MAKINI NA WATU WA KARIBU.

Ujenzi ni kati ya kazi zenye changamoto sana linapokuja suala la kudili na watu wanaofanya kazi hizi za ujenzi kwa sababu ni eneo linahusisha pesa hivyo watu huingiza sana hisia hasa hisia za tamaa na kusababisha zoezi zima kuwa na changamoto kubwa kwenye kudili nalo.

Lakini hakuna kitu kigumu kama kudili na watu ambao wana mipango mingine ya chini chini usiyoijua hasa amba huwafahamu kiundani na hujui mipango yao, jambo hili huleta madhara makubwa sana linapokuja suala la ujenzi na mara nyingi wewe huishia kudanganywa bila kujua nini kinachoendelea.

WATU WAAMINIFU NA WA KUAMINIKA WAPO, JAPO NI WACHACHE

Suluhisho la changamoto hii ambayo usipokuwa nayo makini itakuingiza kwenye hasara, hatari ya kazi mbovu na uhasama na watu ni kuwa makini sana na watu unaofanya nao kazi ambapo unatakiwa uhakikishe ni watu wa kuaminika. Japo watu wasio waaminifu ni wengi sana lakini bado watu waaminifu na wa kuaminika wapo na japo ni wachache lakini wanajulikana, na kwa sababu uaminifu ni tabia basi unaweza kuwaamini na kufanya kazi ukiwa na utulivu mkubwa na kupata matokeo unayotarajia.

UAMINIFU NI TABIA HIVYO UKIFANYA KAZI NA WATU WAAMINIFU UNAWEZA KUPATA UTULIVU NA KUPATA MATOKEO UNAYOTEGEMEA

Watu wa kuwa nao makini zaidi ni watu wa karibu, kama ndugu jamaa na marafiki. Watu wa karibu ni watu unaowafahamu na kwa sababu tu unawafahamu utajikuta unafanya kosa la kuwaamini bila kujali tabia zao halisi ambazo pengine huzifahamu. Ni rahisi kujikuta ukiangukia kwa watu wa karibu kwa sababu ni watu waliokuzunguka muda wote na ambao wanafahamu mambo yako hivyo hata wao wanaweza kuwa wanawinda nafasi za kufanya kazi zako kwa sababu wanajua mambo mengi yanayokuhusu. Lakini tunachosahau ni kwamba watu wa karibu pia wana tabia nzuri na mbaya kama watu wengine, ni watu pia wenye tamaa na tabia nyingine zinazoweza kukuumiza, na kikubwa zaidi ni kwamba watu wa karibu wanakumudu, wanajua udhaifu wako na uimara wako, wanajua mienendo yako na mambo unayopenda au kutokupenda hivyo wanajua namna ya kucheza na wewe vizuri zaidi kuliko watu mbali.

WATU WA KARIBU WANAKUFAHAMU KWA UNDANI ZAIDI KULIKO WATU WA MBALI, HIVYO WAKO KWENYE NAFASI NZURI YA KUKUGHARIMU ZAIDI

Hivyo japo watu wa karibu ambao wana tabia nzuri na wanaweza kukufanyia kazi kwa umakini lakini kama huna uzoefu nao watu wa karibu wanaweza kuwa ni hatari kuliko watu wa mbali, na kibaya zaidi watu wa karibu wanaweza hata kukuletea taarifa za upotoshaji juu ya mtu mwingine asiye wa karibu ulimpa kazi ili waweke wa kwao na kupelekea kuharibu kabisa kazi jambo ambalo unaweza kuja kuligundua kwa kuchelewa au hata usigundue kabisa.

Muhimu ni kufanya kazi na watu wenye uwezo mkubwa na wanaoaminika na ujue namna ya kudili nao kwa usahihi huku ukiwa makini na kila taarifa unayopokea kutoka kwa mtu yeyote.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *