NI MUHIMU SANA KUZINGATIA UJENZI BORA KUEPUKA HASARA NA USUMBUFU
Tunahitaji kukumbushana sana kuhusu kuzingatia ujenzi bora kabla mtu hajaanza mradi wa ujenzi kwa kufanya maamuzi sahihi na uchaguzi sahihi juu ya namna anaenda kufanikisha mradi wake kwa kufanya kazi na watu sahihi na kwa namna sahihi na kwa viwango sahihi. Hasara na usumbufu ambavyo vinaletwa na ujenzi holela na kufanya kazi na watu wasio sahihi hasa kwa upande wa kitaaluma humbatana na majuto ya maumivu makala na gharama mpya za kurudia katika kurekebisha uharibifu uliofanyika.
Kuzingatia ujenzi bora kutakupa utulivu mkubwa ambao unaweza usiouone pale mambo yanapokuwa yameenda vizuri ila mambo yatakapokwenda vibaya ndio utajua thamani ya kufanya kazi na watu makini lakini kwa kupitia njia ngumu baada ya kuwa umepitia usumbufu, mateso, majuto, maumivu makali na hasara kwa kufanya uzembe kwenye jambo linalogharimu sehemu kubwa ya maisha yako ya kifedha.
Kuzingatia ubora kwenye ujenzi ni pamoja na kufanya kazi na watu makini kuanzia kwenye michoro ya ramani, kuzingatia ushauri wa kitaalamu huku ukijaribu kutafuta uwiano na hisia zako nyingine binafsi katika kupata matokeo unayoyatazamia au kuyatamania. Kufanya ujenzi na watu sahihi huku ukiepuka kuendeshwa na hisia mbalimbali badala yake kufikiri kwa makini na kwa usahihi juu ya faid ana madhara maamuzi yoyote unayofikia katika kufanikisha kile hasa unachotamani. Uzuri wa maamuzi sahihi ni kwamba mwisho wa siku yatakupa furaha, amani na kujivunia kile ulichofanikisha.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!