USICHOKIJUA KUHUSU KUPENDA URAHISI.

Ni asili ya binadamu kupenda vitu rahisi na vya mkato kwa sababu vinatupa unafuu wa kufanikisha jambo bila kuumia au kuteseka sana. Rahisi inashawishi kwamba unaweza kufanya jambo kubwa kwa kiasi kidogo cha rasilimali hivyo unapunguza kujihangaisha zaidi, hii ni asili ambayo ubongo ulijitengenezea tangu zamani hivyo mtu anavyosikia rahisi anasikia kupata unafuu na hisia zake kwa haraka zinamsukuma kutumia fursa hiyo kufanikisha jambo lake haraka.

HISIA ZINAKUPA KURIDHIKA KISAIKOLOJIA LAKINI UHALISIA UNAKUONYESHA KINACHOWEZEKANA

Lakini kwa bahati mbaya hisia na uhalisia ni vitu viwili tofauti, wakati hisia zetu zinapenda rahisi na kuvutiwa haraka kukimbilia kwenye rahisi, katika uhalisia rahisi huambatana na matatizo yake mengi ya huo urahisi wenyewe. Mara nyingi inakuwa ni rahisi kwa sababu thamani inayowekwa ni kidogo kwa maana ya kwamba kama ni huduma basi muda unaowekwa katika kutoa huduma husika ni mchache hivyo mwisho wa siku huduma hiyo inakuwa ni ya juu juu tu, kwa mfano kama ni mtu anafagia eneo basi anafagia juu juu na kwa haraka haraka hivyo anaacha uchafu mwingi nyuma au kuna maeneo yaliyojificha hatayafagia. Au wakati mwingine ni watu anaowachukua kufagia naye ni watu wasio na uzoefu na hawakuwa na kazi kwa hiyo anawapata kwa bei rahisi kuwatumia kufagia ndio maana hata gharama yake imekuwa ni rahisi.

Kwenye ujenzi napo kanuni ya asili nayo haikwepeki kwamba unapokutana na urahisi wa aina yoyote, iwe ni kwenye malighafi au kwenye ufundi unapaswa kujiuliza na kufuatilia kwa undani ubora na viwango vya malighafi au huduma husika kwani mara nyingi kuna ukaribiano mkubwa kati ya vitu hivi. Wewe utafurahia urahisi kwa sababu unakufanya kujisikia vizuri kihisia kutokana na ule unafuu unaopata, huku naye aliyepewa kazi akijisikia vizuri kutokana na fedha anayokwenda kuingiza inayomtoa kwenye ukata alionao na kumpa unafuu wa maisha lakini katika uhalisia pengine uwezo wake na wale waliomzunguka sio mkubwa kiasi cha kutosha kukupatia kazi yenye viwango unavyovitarajia.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *